Na Mwandishi – Morogoro
Shirika la Posta Tanzania limeshiriki Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani, ambapo kitaifa yamefanyika Mkoani Morogoro.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu inayosema _”Mishahara Bora na Ajira za Staha ni Nguzo kwa Maendeleo ya Wafanyakazi Wakati ni Sasa”_ yalianzia viwanja vya Shule ya Sekondari Morogoro na kuhitimishwa katika uwanja wa Jamhuri ambako ndiko kilele cha maadhimisho hayo yalipofanyika.
Mgeni Rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Imetolewa na;
Kitengo cha Mawasiliano
Shirika la Posta Tanzania
01 Mei 2023