Geita Gold FC Kutokea Mkoani Geita kupitia Mtendaji Mkuu wa Geita Gold Simon Shija, amekanusha taarifa za kuuza Mechi inayotarajiwa kuchezwa siku ya Jumapili kati yao na Yanga utakaochezwa uwanja CCM Kirumba, Mwanza.
Akizungumza na wandishi wa habari, Shija amesema lengo la kupeleka mechi hiyo katika Dimba la CCM kirumba ni kutokana na Masuala ya kiusalama kuhofia mashabiki kujaa endapo wangechezea katika Dimba lao la Nyankumbu Mkoani Geita.
Aidha Shija amewataka mashabiki kuendelea kujitokeza kwa wingi kununua tiketi katika maeneo mbalimbali huku akiwataka kuja katika dimba la CCM kirumba kushabikia timu yao.