Featured Kitaifa

MBUNGE NEEMA LUGANGIRA ATAKA MAJI TAKA YENYE ZEBAKI YASIINGIE ZIWA VICTORIA

Written by mzalendoeditor

Kamati ya Bunge ya Ukimwi,
Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza wakiwa kwenye picha ya pamoja

MJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi,
Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza Neema Lugangira

NA MWANDISHI WETU, GEITA.

 

MJUMBE wa Kamati ya Bunge ya Ukimwi,
Kifua Kikuu, Madawa ya Kulevya na Magonjwa Yasiyoambukiza Neema Lugangira ametaka
maji taka yenye zebaki yasiingie kwenye ziwa Victoria kutokana na kuwa na
athari kwa binadamu.

 

Mbunge Lugangira aliyasema hayo
wakati wa kamati hiyo ilipotembelea Mgodi wa Geita Gold Mine (GGM) na hilo
linatokana na kudaiwa Maji Taka kutoka Migodini inaingia Ziwa Victoria na ina
Kemikali ya Zebaki nyingi hatua ambayo ndio kiini cha ongezeko kubwa sana la
magonjwa ya Kansa kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa ikiwemo na Kagera anapotokea
mbunge huyo

 

Akijibu hoja hiyo Naibu Waziri wa
Afya Dkt Godwin Molel alikiri ni kweli ukienda Hospitali ya Ocean Road wagonjwa
wengi wa Kansa wanatoka Mikoa ya Kanda ya Ziwa hivyo aliahidi kuwa Wizara ya
Afya kufanya Utafiti kujua nini kinasabisha tatizo la Magonwa ya Kansa kukua
kwa kasi kubwa Mikoa ya Kanda ya Ziwa.

 

 

Kwa upande wake Naibu Waziri wa
Wizara ya Madini, Mhe Dkt.Steven Kiruswa aliichukua changamoto hiyo na kuhaidi kwamba
Serikali inachukulia jambo hili kwa uzito mkubwa na tayari imeshaweka mikakati
kambambe ya kuhakikisha ifikapo mwaka 2029 Serikali itakuwa imekomesha kabisa
matumizi ya Kemikali ya Zebaki.

About the author

mzalendoeditor