Featured Kitaifa

TASAF: UTAMBUZI KAYA MASIKINI 169 ZAANDIKISHWA KUPATA RUZUKU

Written by mzalendoeditor

 

Utaratibu wa kutambua kaya maskini  na kuzifanyia uhakiki ulifanywa kwa kushirikiana na ustawi wa jamii na ofisi ya Waziri mkuu ambapo kaya zaidi ya 169.000 ziliandikishwa na zinapata Ruzuku.

Katika kila kundi la watu wenye Ulemavu leo wameweza kutoa maoni yao huku ushirikishwaji wa viongozi kila aina ya wenye Ulemavu hii italeta mafanikio makubwa zaidi ya utekelezaji wa shughuli hizi katika vyama hivyo na kuturahisishia kazi ya utambuzi.

Hayo yameelezwa na Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF Ladislaus Mwamanga alipokutana na  viongozi  kaya masikini zaidi ya Hamsini kutoka vyama mbali mbali  pamoja na wawakilishi kutoka ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar mwishoni mwa wiki hii ili kupata mawazo tofauti juu ya uboreshaji na utekelezaji wa kazi za TASAF katika kusaidia watu kutoka katika kaya maskini.

TASAF Imekuwa pia ikitoa elimu kwa kaya maskini juu ya Elimu Afya na lishe pamoja na kuhamasisha vikundi vya kuweka akiba na kuwekeza ili walengwa fedha wanazozipata kutoka TASAF waweze kuziingiza kwenye uzalishaji na kuanzisha shughuli za kiuchumi zinazolingana na mahitaji yao kama kilimo, Ufugaji na Biashara ndogo ndogo.

Kuhusu suala la kuhitimu baadhi wa watu wanakuwa wagumu kujitoa japo maisha yao yameshaimarika tayari kupita changamoto hiyo TASAF wameshafanya uhakika na zile kaya ambazo zimeimarika zinatakiwa kujitoa huku kaya chache zikiwa tayari zimejitoa kwenye mradi huo kwa hiyari baada ya maisha yao kuimarika huku wakiishukuru serikali kwa kuwatambua na kwamba wameamua kujitoa kupisha kaya zingine za wahitaji kuingia kwenye mradi huo.

Aidha mkurugenzi huyo amesema msingi mkubwa wa programu hiyo ni kuwajengea uwezo katika kaya zinazosaidiwa ili wafanye maamuzi yao kuhusu mambo yao mbalimbali ikwepo Bima za Afya na TASAF inawahamasisha kila wanapopokea hela kujiwekea kiasi kwa ajili ya Bima.

Hata hivyo serikali kupitia TASAF wameanza kutafuta takwimu kujua kaya maskini za wenye ulemavu zipo ngapi ili waweze kuwapa bima za Afya.

Ameongeza kwamba baadhi ya kaya maskini tayari wameshakata bima za Afya kupitia fedha za kujikimu wanazopewa kupitia mfuko wa TASAF na wameweza pia kukopeshana wenyewe kwa wenyewe.

About the author

mzalendoeditor