Featured Kitaifa

MBUNGE MTATURU AIKUMBUSHA SERIKALI KULIPA WASTAAFU.

Written by mzalendoeditor

MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu ,ameendeleza kilio chake cha kucheleweshwa kwa mafao ya wastaafu ambapo safari hii ameikabidhi serikali barua yam zee Simon Albert Makiya kwa ajili ya utekelezaji.

Mei 2022,katika swali lake la msingi Mtaturu aliihoji serikali lini itamaliza changamoto ya kucheleweshewa mafao kwa wastaafu ambapo serikali ilieleza jitihada zake ikiwemo kulipa deni la mfuko wa PSSSF ikiwa ni pamoja na kutoa hatifungani ya Shilingi Trilioni 2.17 ambazo zitaimarisha mtiririko wa mapato na kuwezesha kutoa mafao kwa wakati.

Aidha,Mei 2020,akichangia mjadala wa bajeti ya wizara ya fedha na mipango,Mtaturu aliiomba serikali kuwalipa mapema wastaafu mafao yao na kuwataja wazee wawili wa Ikungi Mohammed Ntandu na Gamilliel Massawe suala ambalo serikali iliahidi kulishughulikia.

Leo April 13,2023,ni mara ya tatu kutoa kilio hicho,“Eneo hili limekuwa likilalamikiwa sana na wabunge wamepata malalalmiko hayo,kuna mzee wangu mmoja ambaye barua yake ninayo ameniletea kama mbunge wake Simon Albert Makiya kutoka Siuyu,

“Barua hii nitaomba niikabidhi kwa waziri,mzee huyu amekuwa akilalamika anasubiri fedha zake za kustaafu na amekuwa akija hapa bungeni akifanya juhudi za kumuona waziri ili asikilize kilio chake,naomba watu wa aina hii watendewe haki ,”amesisitiza.

About the author

mzalendoeditor