Featured Michezo

YANGA SC YAJIPINGIA NJE NDANI TP MAZEMBE CAF

Written by mzalendoeditor

Na.Alex Sonna
WAWAKILISHI Pekee katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Timu ya Yanga SC imeendelea kujipingia na kulipa kisasi cha mwaka 2016 baada ya kuichapa tena TP Mazembe bao 1-0 mchezo uliopigwa uwanja wa Stade TP Mazembe  Mjini Lubumbashi nchini DR Congo.
 
Shujaa wa Yanga SC ni kiungo mshambuliaji aliyetokea benchi Farid Musa alifunga bao hilo dakika ya 63 akimaliza pasi ya Jesus Moloko kwa ushindi huo Yanga imelipa kisasi cha mwaka 2016 ambapo walifungwa na Mazembe nje ndani wakifungwa Benjamin bao 1-0 na kufungwa tena nchini DR Congo mabao 3-1.
 
Kwa ushindi huo Yanga wamefikisha Pointi 13 na kuongoza kundi huku wakisubiria mchezo kati ya US Monastir wenye Pointi 10 watakaovaana na Real Bamako majira ya saa tano usiku.
Licha ya Yanga kuwakosa nyoka wake wa kikosi cha kwanza ambapo  Djidji Diara, Khalid Aucho, Aziz Ki na Morrison  pamoja na Kocha wao Prof,Nabii haikuwazuia kuibuka na ushindi huo.

About the author

mzalendoeditor