Kitaifa

SERIKALI YAVIAGIZA VYUO VYA UALIMU KUTUNZA MAZINGIRA 

Written by mzalendoeditor

KAIMU  Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe akizungumza wakati akifungua mafunzo  ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP)  leo Februari 23,2023,Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.

MKURUGENZI  msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Bw.Huruma Mageni, akitoa taarifa ya  mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu  (TESP)leo Februari 23,2023,Wilayani  Mpwapwa , Mkoani Dodoma.

MRATIBU Mshauri Elekezi wa Mradi wa Kuendeleza Elimu ya Ualimu (TESP) kutoka nchini Canada Bi.Alix Yule, akizungumza wakati ya  mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu  (TESP)leo Februari 23,2023,Wilayani  Mpwapwa , Mkoani Dodoma.

MRATIBU wa Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu  (TESP) Bw.Cosmas Mahenge,akizungumza wakati ya  mafunzo ya siku nne ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu  (TESP)leo Februari 23,2023,Wilayani  Mpwapwa , Mkoani Dodoma.

SEHEMU ya washiriki wakimsikiliza Kaimu  Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe (hayupo pichani) wakati akifungua mafunzo  ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP)  leo Februari 23,2023,Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.

MWENYEKITI wa Wakuu wa Vyuo Taifa Bw.Agustino Sahili,akitoa neno la shukrani kwa Mgeni rasmi Kaimu Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe (hayupo pichani) mara baada ya kufungua mafunzo  ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP)  leo Februari 23,2023,Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.

KAIMU  Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua mafunzo  ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP)  leo Februari 23,2023,Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.

 

KAIMU  Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.James Mdoe,akipanda mti katika chuo cha ualimu Mpwapwa mara baada ya kufungua mafunzo  ya utunzaji wa mazingira endelevu na ujanishaji kwa wakufunzi na menejimenti ya vyuo vya ualimu ,yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu  kupitia Mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu (TESP)  leo Februari 23,2023,Wilayani Mpwapwa ,Mkoani Dodoma.

Na.Alex Sonna-MPWAPWA

SERIKALI imevitaka vyuo vya ualimu nchini kutunza mazingira na kuangalia namna bora ya matumizi ya  nishati ya kupikia ikiwemo utumiaji wa kuni.

Hayo yameelezwa leo Februari 23,2023 Wilayani Mpwapwa Mkoani Dodoma na Kaimu  Katibu Mkuu Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia,Prof.James Mdoe,wakati akifungua mafunzo ya utunzaji mazingira endelevu na  ujanishaji kwa wanafunzi na Menejimenti ya Chuo cha Ualimu Mpwapwa.

Prof. Mdoe, amesema kutokana na matumizi ya teknolojia wanatakiwa kutoka katika matumizi ya kuni ama kuanzisha mashamba maalum katika vyuo kwa ajili ya kuvuna kuni lengo likiwa ni kutunza mazingira.

“Matumaini yangu tutatumia namna ya kupunguza bajeti ya matumizi ya nishati aidha kwa kuboresha au kuangalia aina ya majiko tunayotumia lakini kupunguza bajeti ya matumizi ya nishati,mimi matamanio yangu tudhibiti uharibifu wa mazingira.

“Mnakuwa na shamba lenu ambalo mnavuna hapa hapa kama tumeamua kutumia kuni,kuna wengine wanafanya watupe uzoefu na tuwe tayari kuuchukua.

“Baadhi hatupo tayari kubadilika tunafanya kwa nadharia tu, tuwe tayari kubadilika,”amesema Prof. Mdoe, 

Aidha amewataka kujifunza namna ya kuandaa mpango kazi  wa muongozo na unatekelezwaje  kulingana na mahitaji ya rasilimali fedha kwani  kuna utofauti kulingana na chuo na chuo.

Prof. Mdoe, amesema vyuo vinatakiwa kuhamasisha upandaji wa mti hasa katika mzimu wa mvua ili kutunza mazngira.

 Amesema wazee wa zamani bado wana kasumba ya kupanda miti kila inapofika msimu wa mvua hivyo wakufunzi hao wanatakiwa kuhakikisha wanasimamia zoezi la upandaji wa mti.

Pia amewapata kuhakikisha  wanatoe elimu ya utunzaji wa mazingira kwa walimu watarajiwa ili na wao wakafundishe wanafunzi watakaokuwa wakiwafundisha.

“Wangapi bado tunaendelea kupanda miti hapa Mpwapwa sina malalamiko lakini Je wote mnafanya hivyo? Ili tuweze kutunza  mazingira na kuboresha mandhari,”amesema Prof. Mdoe

Amesema mafunzo hayo yanatolewa kwa siku nne na yatagusa maeneo manne ikiwa ni pamoja na ukijanishaji  katika vyuo.

Amesema mafunzo hayo yanahusu vyuo 35 vya ualimu ambapo jumla ya vyuo  14 vimeishapata mafunzo hayo.

“Sasa  ni zamu yenu sasa napenda niwakaribishe sana na nichukue fursa hii kuwapongeza walioandaa mafunzo haya.Mimi binafsi ninamatumani makubwa kwamba mafunzo haya yatatujenga kwa sababu sisi ni wakufunzi tutapata kitu na tutawaanda vizuri walimu tunaowandaa.

“Lengo tunapojifunza mbinu mbalimbali ukijanishaji ni lazima ziingie katika vichwa vyetu na wakufunzi wetu na walimu wanafunzi ili wakienda kule wawasaidie wanafunzi wao,”amesema Prof. Mdoe,

Amesema Serikali inatambua umuhimu  wa utunzaji wa mazingira na katika kuhakikisha hilo limeweka mikakati ikiwemo kulinda  vyanzo  vya maji pamoja na uzuiaji wa ukataji  wa  miti hovyo

Amesema makakati huo utasaidia kupunguza gharama za uendelsahaji wa vyuo huku akidai suala la nishati ya kuni linakula fedha nyingi.

Kwa upande wake Mkurugenzi msaidizi wa Elimu ya Ualimu kutoka Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia Huruma Mageni  amesema Wizara ya Elimu kwa kushirikiana na Serikali ya Canada inatekeleza mradi wa kuendeleza elimu ya ualimu nchini kwa kuboresha mazingira ya kujifundishia na kujifunzia.

Amesema mafunzo  hayo yanalenga kuhakikisha  kunakuwa na mkakati wa utunzaji wa mazingira katika vyuo vya uliamu na usimamaizi wa taka ngumu pamoja na ujenzi rafiki na utunzaji  wa mazingira asili.

“Mafunzo haya yanajumuisha wakuu wa vyuo 35 na wakufunzi ambao watakuwa na jukumu la kusimamia hii program katika vyuo vyao”amesema Mageni

About the author

mzalendoeditor