Na.Alex Sonna-MZALENDO BLOG
WAWAKILISHI katika Michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika Yanga wamevuna shilingi 15 milioni za ahadi iliyotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kununua kila bao moja Sh5 milioni baada ya kuichapa mabao 3-1 TP Mazembe mchezo wa Kundi D uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Mabao ya Yanga yamefungwa na wachezaji waliosajiliwa dirisha dogo la usajili Kenedy Musonda dakika ya 7 na Mudathir Yahya dakika 11.
Kipindi cha Pili Mazembe walipata bao kupitia kwa Alex Ngonga kwa Mpira wa Faulo ulienda moja kwa moja dakika ya 80 na katika dakika ya 90 +2 Tuisila Kisinda alipingilia msumari wa tatu.
Kwa Matokeo hayo Yanga wapata pointi 3 sawa na Mazembe wakiwa na tofauti ya uwiano ya mabao ya kufungwa na kufunga na kushika nafasi ya tatu huku Mazembe akishika nafasi ya pili ,nafasi ya kwanza inashikwa na US Monastir wenye pointi 4 baada ya kupata sare dhidi ya AS Real Bamko ambao wanshika mkia wakiwa pointi 1