Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AWATAKA WAKANDARASI KUFANYA KAZI KWA UFANISI

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi wa Shirika la Umeme nchini TANESCO Maharage Chande akiwa pamoja na Mwanasheria wa Shirika hilo Zaharani Kisilwa wakati wakitia saini Mikataba mbalimbali ya Gridi Imara na Wakandarasi mbalimbali kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akishuhudia Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Umeme Vijijini REA Eng. Hassan Saidy pamoja na Mwanasheria wa REA Mussa Muze wakati wakitia saini Mikataba ya kupeleka Umeme maeneo mbalimbali nchini kwenye hafla iliyofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023. 

– Advertisement –

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Viongozi mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9. Hafla ya utiaji saini Mikataba ya kuimarisha Gridi ya Taifa na usambazaji wa umeme Vijijini imefanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akiwa kwenye picha ya pamoja na wageni mbalimbali mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9, Ikulu Jijini Dar es Salaam 

Wageni mbalimbali wakiwa kwenye hafla ya Utiaji Saini wa Mikataba 26 ya Gridi Imara yenye thamani ya Shilingi Trillion 1.9 Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Februari, 2023.

************************

 

– Advertisement –

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Wakandarasi wazawa walioshinda zabuni kuhakikisha kufanya kazi zenye ubora kwa ufanisi, uaminifu na kufuata makubaliano yaliyofikiwa katika mikataba.

Rais Samia ametoa wito huo leo wakati akishuhudia utiaji saini mikataba ya kuimarisha gridi ya taifa na kusambaza umeme vijijini katika hafla iliyofanyika Ikulu.

Aidha, Rais Samia amewataka Wakandarasi waliokosa kandarasi kuridhika na maamuzi ya zabuni yaliyoamuliwa kwa kuwa kupinga maamuzi hayo kunachelewesha kuanza kwa miradi iliyopitishwa

– Advertisement –

Vile vile, Rais Samia amezitaka Wizara zinazohusika na malipo ya Wakandarasi wa miradi kuhakikisha wanawalipa kwa wakati pindi wanapokamilisha kazi zao.

Aidha, Rais Samia amesema miradi hii yenye thamani ya shilingi trilioni 1.9 ni ya muhimu kwa wananchi kwa kuwa itaimarisha huduma za maji, kilimo, afya na hivyo kuleta maendeleo.

Shirika la Umeme (TANESCO) limeweka saini mikataba 6 kwa ajili ya miradi 26 ya gridi imara na Wakala wa Umeme Vijijini (REA) imeweka saini mikataba 14 kwa ajili ya miradi ya kupeleka umeme kwenye migodi midogomidogo na maeneo ya kilimo.

Miradi hiyo itapeleka umeme katika maeneo 336 ya uzalishaji mali, vitongoji 1522, vituo vya afya 65 na maeneo 336 yenye vyanzo vya maji ili kujenga uchumi, kuongeza uwekezaji na utoaji huduma za jamii katika ngazi za chini.

About the author

mzalendoeditor