Na Okuly Julius-Dodoma
Shule ya MAKI BRILLIANT iliyopo Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino Mkoani Dodoma inawakaribisha Wazazi na Walezi wote Siku ya Jumamosi Disemba 10,2022 kushiriki sherehe maalum itakayofanyika Shuleni hapo.
MAKI BRILLIANT PRE AND PRIMARY ENGLISH SCHOOL imesajiliwa Feb 28 ,2022 ikiwa na wanafunzi tisa (9) ambapo hadi kufikia sasa wana jumla ya wanafunzi 60 kuanzia darasa la kwanza mpaka darasa la Sita.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Leo Desemba 8,2022, Jijini Dodoma kuelekea Sherehe hiyo ,Afisa Masoko na Mawasiliano wa Shule hiyo Bi.Josephine Uriyo amesema kuwa lengo la Sherehe hiyo ni kuwakutanisha kwa pamoja wazazi,Walezi,Walimu na wanafunzi ili wapate kujua na kujionea maendeleo ya Watoto wao ikiwemo vipaji mbalimbali.
“Wanafunzi watakuwa na michezo mbalimbali ambapo watapata nafasi ya kuonesha mbele ya wazazi kwa sababu kuna baadhi ya wazazi hawajui kabisa vipaji walivyonavyo watoto wao ila kupitia Sherehe kama hii itakayofanyika Jumamosi ukweli wazazi watafurahia sana,”Amesema Josephine
Bi.Josephine ametoa wito kwa Wazazi na Walezi kutambua umuhimu wa siku hiyo kwa kushiriki na watoto wao ili kujua maendeleo yao ya msingi ya kielimu pamoja na kimaadili.
“Moja ya sifa ya shule yetu inawalea Watoto katika maadili ya Dini na Uzalendo na imekuwa ikifanya vizuri katika matokeo na ufaulu na tuna nyongeza ya kufundisha watoto Kifaransa na Kichina,”
Na Kuongeza kuwa ‘Shule yetu pia inatoa Elimu ya awali,yaani Nursery School (Baby,Middle na Pre-Unit) na inapokea watoto kuanzia umri wa miaka mitatu (3) na shule yetu inafuata mtaala wa Wizara ya Elimu,SayansinaTeknolojia ,”Amesema Bi.Josephine
Pia Bi.Josephine amesema kuwa Shule ya MAKI BRILLIANT inapokea watoto kuanzia miaka Mitano (5) na kuendelea kwa darasa la kwanza (01) hadi darasa la sita (6).
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri ,Kenneth Yindi amesema kuwa Kata yake Imefungua milango kwa Wawekezaji kwa kiasi kikubwa huku akitolea mfano Shule ya MAKI BRILLIANT kuwa imeongeza idadi kubwa ya Wanafunzi na hayo ni mafanikio ya baadae katika kata yake na taifa kwa ujumla.
“Baada ya Serikali kutangaza kuhamia rasmi Dodoma, Wawekezaji nao wakafunguka na kutaka kuwekeza Dodoma hasa katika Wilaya yetu ya Chamwino ambapo ndipo ilipo Ikulu ya Tanzania na kwa bahati nzuri kata yangu nayo ipo Chamwino hivyo kwa sasa Wawekezaji wengi wanakuja na Mimi kama Diwani nawakaribisha na milango ipo wazi,”Amesema Yindi
Uwekezaji Uliofanyika katika kata yake ikiwemo Ujenzi Wa Shule ya MAKI BRILLIANT umeleta maendeleo makubwa kwa Watoto wa kata hiyo kwani wengi wao sasa wanapata elimu bora na yenye maadili hivyo kikubwa ni kuendelea kuwaunga mkono Wawekezaji wanaoendelea kuwekeza katika miradi ya maendeleo ikiwemo hizi shule kwa sababu ni msingi wa watoto kupata elimu.
Lengo la Kuanzishwa kwa shule ya MAKI BRILLIANT katika Kata ya Buigiri Wilayani Chamwino ni kuwasaidia watoto wa kika na wakiume kupata elimu Bora ili kuibui vijana walioelimika na wenye maadili mema pamoja na kuwafundisha ujasiriamali hali ambayo itawasaidia katika maisha yao ya baadae.