Featured Kitaifa

PROF. MKENDA APONGEZA WADAU KWA NAMNA WANAVYOLETA MAGEUZI KATIKA SEKTA YA ELIMU.

Written by mzalendoeditor

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu  wenye lengo la kutoa fursa kwa wadau mbalimbali wa elimu kushiriki kikamilifu katika kupanga Mipango ya Maendeleo ya Elimu na Programu kwa ajili ya kuleta maendeleo endelevu kwa mtu mmoja mmoja, jamii na taifa kwa ujumla unaofanyika kwa siku mbili kuanzia Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael,akizungumza wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

SEHEMU ya Wadau wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu pamoja na wanafunzi wakifatilia mada mbalimbali wakati wa  Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba   6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu Tanzania  Bi.Faith Shayo,akitoa maoni wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

Mratibu wa Kitaifa wa Mtandao wa Elimu Tanzania Bw.Ocholo Wayoga,akizungumza  wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Francis Michael,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki wakati wa Mkutano wa Mwaka wa kufanya Mapitio ya Sekta ya Elimu unaofanyika kwa siku mbili kuanzia leo Disemba 6 mpaka 7 Jijini Dodoma.

……………………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI  wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda ,amesema Mwamko wa kufanya mageuzi ya elimu ni ajenda iliyopo Duniani kote na  kwamba Tanzania imewahi kuanza mageuzi hayo.

Hayo ameyasema leo Disemba 6,2022 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa mwaka wa kufanya mapitio ya Sekta ya elimu ambapo amewaomba wadau hao kushiriki katika mageuzi hayo.

Prof.Mkenda amewapongeza wadau kwa namna wanavyoshiriki kikamilifu kutoa maoni yao madhubuti kwa ajili ya kusaidia Mageuzi Makubwa katika sekta ya Elimu nchini.

”Sekata ya Elimu  nchini bado inahitaji mageuzi makubwa hivyo anaamini kupitia mkutano huo Wadau watapata nafasi ya kujadi kikamilifu namna ya kuleta maendeleo endelevu kwenye sekta ya Elimu.

“Baada ya Rais Samia kuingia madarakani alitoa maelekezo ya kufanya mapitio ya Sera na mabadiliko ya mitaala kwa lengo la kuhakikisha elimu inayotolewa inaendelea kuwa bora na kutoa elimu ujuzi. Niwaombe wadau tuendelee kushirikiana katika kuboresha na kukuza elimu nchini,” amesema Prof Mkenda.

Aidha Waziri Mkenda amewataka wadau hao kuwa mapitio ya sera na mitaala yameshirikisha wadau mbalimbali na kwamba kwa sasa yapo tayari kwa mjadala wa kitaifa kuhusu mapendekezo ya sera ya elimu na mitaala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt.Francis Michael  amesema kila mmoja aliyepata fusa ya kushiriki mkutano huu kujadili kwa kina mada zitakazowasilishwa na kutoa maoni yenye tija katika kuimarisha na kuendeleza elimu yetu nchini.
” Wizara inaendelea na maboresho ya mitaala kuanzia ngazi ya Elimumsingi hadi Elimu ya juu,uboreshaji wa Sera ya Elimu unaendelea baada ya ukusanyaji wa maoni ya wadau wa elimu nchini kote na kuendelea kuyachakata,”Amesema Dkt.Michael
Pia Dkt.Michael amesema Kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania imeandaa miongozo ya utoaji wa elimu kwa kutumia TEHAMA kwa elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu na Kukamilisha Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu 2021/22 -2025/26.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wadau wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu Tanzania  Bi.Faith Shayo amesema kuwa Mkutano huo umekuja Muda Muafaka kwani Dunia kupitia Umoja wa Mataifa ipo katika mabadiliko na mageuzi katika Sekta ya elimu kuanzia Sera,Miongozo na Mitaala yake ili kuleta mageuzi yenye tija.

About the author

mzalendoeditor