Featured Michezo

WATUMISHI TUME YA MADINI WASHIRIKI BONANZA LA MICHEZO NA WATUMISHI WA CHUO CHA MIPANGO

Written by mzalendoeditor

 

MWENYEKITI wa Tume ya Madini Prof. Idrisa Kikula,(liyevaa Kofia) akishiriki katika   matembezi pamoja na watumishi wa tume hiyo kushirika Bonanza kuelekea katika Shule ya Sekondari John Merine kushiriki Michezo mbalimbali leo Desemba 3,2022 jijini Dodoma. 

MWENYEKITI wa Tume ya Madini Prof. Idrisa Kikula,(liyevaa Kofia) akiwaongoza watumishi wa tume hiyo kushirika mazoezi mbalimbali wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma. 

WACHEZAJI wa Timu za Mpira wa Miguu kati ya Watumishi wa Tume ya Madini wakichuana na Watumishi wa Chuo cha Mipango ambapo Tume ya Madini wameibuka na ushindi wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma. 

 

MWENYEKITI wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula,(liyevaa Kofia) akiwa na Kamishna wa Tume ya Madini,Janet Lekashingo wakitazama mechi kati ya Watumishi wa Tume ya Madini wakichuana na Watumishi wa Chuo cha Mipango ambapo Tume ya Madini wameibuka na ushindi wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma. 

 Watumishi wa Tume ya Madini wakichuana na Watumishi wa Chuo cha Mipango katika Mpira wa Pete  wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma.

MWENYEKITI wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula,akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba na Kushoto ni Kamishna wa Tume ya Madini,Janet Lekashingo.

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Yahya Samamba,akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma lililoshirikisha watumishi wa Tume ya Madini na Watumishi wa Chuo cha Mipango.

Kamishna wa Tume ya Madini,Janet Lekashingo ,akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma lililoshirikisha watumishi wa Tume ya Madini na Watumishi wa Chuo cha Mipango.

MWAKILISHI wa Watumishi wa Chuo cha Mipango,akizungumza wakati wa Bonanza la Michezo lililofanyika leo Desemba 3,2022 katika Shule ya Sekondari John Merine  jijini Dodoma

……………………………..

Na Alex Sonna-DODOMA

MWENYEKITI wa Tume ya Madini Prof. Idris Kikula amewaongozo watumishi wa tume hiyo kushiriki Bonaza la Michezo mbalimbali likiwa na lengo la kuboresha afya zao ili kujikinga na Magonjwa mbalimbali pamoja na kuongeza mshikamano wakati wanapotimiza wajibu wao.

Akizungumza leo Desemba 2,2022 wakati wa Bonanza hilo lililofanyika katika Shule ya Sekondari John Merine jijini Dodoma  Mwenyekiti wa Tume hiyo Prof. Kikula amesema bonanza hilo limetumika katika kuboresha afya pia linatumika kuhamasishana wafanyakazi wa tume kuchapa kazi ili kufikia malengo ya ukusanyaji maduhuli.

Prof.Kikula amesema watumishi wameona umuhimu wa kufanya mazoezi ili kuondokana na magonjwa yasiyoambukiza kwa changamoto kubwa kwani watumishi wa umma wamekuwa hawafanyi mazoezi mara kwa mara.

”Bonanza kama hilo ambalo linafanyika mara ya nne limekuwa likitumika kuweka afya vizuri na kufahamiana lakini pia linaondoa ukuta baina ya wafanyakazi na viongozi wao.”amesema Prof.Kikula

Aidha amesema kuwa Tume  imepewa malengo ya kukusanya maduhuli ya serikali ya sh bilioni 822, hivyo imetumia bonanza hili pamoja na kuweka afya vizuri pia kuhamasishana wafanyakazi kufanya kazi kwa ufanisi.

”Katika kufikia malengo hayo ya kukusanya maduhuli hayo ambayo wanajipima kwa kukusanya na kuangalia mapato ya kila mwezi na hadi sasa wanaendelea vizuri katika makusanyo hayo na wana uhakika ifikapo Juni 30, 2023 watafikia lengo.”amesema 

Amesema kuwa tume imekuwa ikitumia mikoa ya kimadini inayofikia 47 ambayo baadhi ya mikoa ya kiutawala kama Geita na Morogoro imegawanywa kutokana na ukubwa wake, pia nayo imewekwa malengo katika ukusanyaji huo.

Kwa upande wake Kamishna wa Tume ya Madini, Janet Lekashingo amesema kuwa bonanza hilo pamoja na kuleta afya njema pia linahamasisha wafanyakazi kufanya kwa ufanisi ili kupata tija na kuongeza utendaji bora na kwa ufanisi.
Naye Ofisa Utimishi Mwandamizi wa Tume ya Madini, Joyce Rweyimamu amesema tume imeamua kushirikiana na taasisi nyingine kama Chuo cha Mipango kuonesha ushirikiano na taasisi nyingine za serikali.
Meneja wa Tehama katika Tume ya Madini, Bernard Ntelya amesema kuwa bonanza hilo linasaidia kujenga afya za watumishi kwani bila afya hakuna tume na tume bila wafanyakazi wenye afya bora hakuna ufanisi.
Katika bonanza hilo wafanyakazi wa Tume walishindana na watumishi wa Chuo cha Mipango katika mpira wa miguu, mpira wa pete na kuvuta kamba pamoja na kufukuza kuku na washindi wakapata zawadi mbalimbali.

About the author

mzalendoeditor