Na Mwandishi Wetu, Dar es salaam
Katika kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani leo tarehe 1 Disemba 2022 Kampuni ya Barron ambao ni wazalishaji na wauzaji wa viatu vya watoto wa shule, wameshiriki kutoa msaada wa viatu jozi 50.
Viatu hivyo vimetolewa kwa watoto wenye maambukizi ya virusi vya UKIMWI katika Hospitali ya Mnazi mmoja Jijini Dar es salaam.
Akizungumza wakati wa kukabidhi viatu hivyo kwa watoto hao, Mkurugenzi wa Kampuni ya Barron Group Bi Jacqueline Kawishe amesema kuwa viatu hivyo vimetolewa na mdau ambaye hakutaka jina lake litajwe ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono mapambano ya serikali dhidi ya UKIMWI.
Bi Kawishe amesema kuwa zawadi hizo zimetolewa kuadhimisha siku ya UKIMWI Duniani zikiambatana na kauli mbiu isemayo “Mpange Mwana, Twende Sawa, Imarisha usawa Kujilinda ni ibada”
Viatu hivyo vimetolewa kwa watoto walio na maambukizi ya virusi vya UKIMWI. Lengo kuu la msaada huo ni kusambaza upendo na kuadhimisha kauli mbiu ya mapambano dhidi ya UKIMWI.
Kwa upande wake mganga mfawidhi katika hospitali ya Mnazi mmoja Dkt Delila Moshi, msimamizi wa maswala ya UKIWMI katika hospitali ya Mnazimoja Dkt Vivian Vesso pamoja na mtawala mkuu wa maswala ya UKIMWI katika hospitali ya Mnazimmoja Dkt Zainabu Mwinyimkuu wamempongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Barron Group Bi Jacqueline Kawishe na wadau mbalimbali nchini kwa kuendelea kujitolea kwa watoto wenye mahitaji mbalimbali hususani watoto wenye maambukizi ya UKIMWI.