OR-TAMISEMI

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Angellah Kairuki amesema Serikali kupitia mradi wa kuboresha miundombinu na kupendezesha miji na Majiji (TACTIC) itapeleka shilingi bilioni 14.4 kwa ajili ya ujenzi wa soko,kituo cha mabasi na ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, mkoani Lindi

Waziri Kairuki ameyasema hayo leo tarehe 1 Disemba, 2022 katika Mkutano wa hadhara wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na wananchi wa Mkoa wa Lindi katika ziara yake ya kikazi mkoani humo.

Amesema shilingi bilioni 4 itaelekezwa katika ujenzi wa stendi ya mabasi na bilioni 4.6 zitaelekezwa kwenye ujenzi wa soko katika Halmashauri ya Manispaa ya Lindi mkoani Lindi

Vilevile Waziri kairuki ameeleza kuwa kupitia mradi huo Serikali itapeleka shilingi bilioni 5.8 kwa ajili ya ujenzi wa barabara katika Manispaa hiyo

Previous articleKAMPUNI YA BARRON YAWASILISHA MSAADA WA VIATU KWA WATOTO WENYE MAAMBUKIZI YA UKIMWI
Next articlePATA HABARI MOTO MOTO KATIKA MAGAZETI YA LEO DECEMBER 2,2022

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here