Featured Michezo

LIVERPOOL YATWAA UBINGWA WA CARABAO CUP KWA MATUTA

Written by mzalendoeditor

TIMU ya Liverpool imefanikiwa kutwaa Kombe la Ligi England, maarufu kama Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 11-10 kufuatia sare ya 0-0 na Chelsea usiku huu Uwanja wa Wembley Jijini London.

Kipa Kepa Arrizabalaga aliyeingia dakika ya 119 maalum kwenda kuokoa mikwaju ya penalti, hakuweza kuokoa hata moja na bahati mbaya zaidi kwake akaenda kupiga juu ya lango penalti yake ya mwisho.
Waliofunga penalti za Liverpool ni  Jamaa Milner,  Fabinho, Virgil van Dijk, Trent Alexander-Arnold,  Mohamed Salah, Diogo Jota,  Divock Origi, Andrew Robertson, Harvey Elliott, Ibrahima Konaté na kipa Caoimhin Kelleher.
Waliofunga penalti za Chelsea ni Marcos Alonso, Romelu Lukaku, Kai Havertz, Jorginho, Antonio Rüdiger, N’Golo Kanté, Timo Werner, Thiago Silva na Trevoh Chalobah.

About the author

mzalendoeditor