Featured Kitaifa

DC SHEKIMWERI ATOA NENO KWA WALIMU WA DODOMA MJINI

Written by mzalendoeditor

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa Dini ya Kiislamu wakati wa  maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa yaliyofanyika leo Februari 27,2022 jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab,akizungumza wakati wa  maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa yaliyofanyika leo Februari 27,2022 jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe.Jabir Shekimweri akiteta jambo na Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab wakati wa  maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa yaliyofanyika leo Februari 27,2022 jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Viongozi mbalimbali wa TAMSYA kutoka mikoa tofauti nchini Tanzania wakipita mbele ya Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa ambayo yamefanyika leo Februari 27,2022 katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.

WAUMINI wa Dini ya Kiislamu wakifatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri  (hayupo pichani)  wakati wa  maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa yaliyofanyika leo Februari 27,2022 jijini Dodoma kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

………………………………………………………

Na Bolgas Odilo-DODOMA

WALIMU wa shule za Msingi na Sekondari Wilaya ya Dodoma mjini wametakiwa kutowabagua wala kuwatenga watoto wa kike wa kiislamu kutokana na uvaaji wa Hijjab  kufanya hivyo ni kinyume cha sheria na taratibu za nchi.

Kauli hiyo imetolewa leo Februari 27,2022 jijini Dodoma na Mkuu wa wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Jabir Shekimweri wakati akizungumza  katika maadhimisho ya siku ya Hijjab kitaifa yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri Dodoma.

Shekimweri amesema kuwa, Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan haina Dini ila inatambua dini zote na haiwezi kuingilia misingi ya imani yeyote.

“Serikali ya awamu ya sita Chini ya Rais wetu Mama Samia haina dini ila inatambua dini zote na haiwezi kuingilia misingi ya imani ya dini yeyote hivyo wanafunzi wote wa kike wa kiislamu wanaruhusiwa kuvaa Hijjab.

“Walimu msiache kuwahimiza wanafunzi wa kike mashuleni hasa kwenye vipindi vya dini kuwa wanapaswa kujistiri, na vazi la stara kwa mtoto wa kike wa kiislamu ni Hijjab.

“Kama kuna shule yeyote itakuwa na tabia hizi za ubaguzi au kunyanyapaa wanafunzi wanaovaa Hijjab basi taarifa zitolewe ili hatua stahiki za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao,” amesema Shekimweri.

Kwa upande wake Sheikh wa Mkoa wa Dodoma Alhaj Mustafa Rajab Shabani ,amewahimiza watoto wa kike wa kiislamu kuendelea kujistiri kwa kuvaa Hijjab kwani kwa kufanya hivyo kutalinda heshima yao pia kuongeza thamani na kuepukana na vishawishi,

About the author

mzalendoeditor