Featured Michezo

YANGA YATINGA HATUA YA MAKUNDI CAF,YAIZAMISHA CLUB AFRICAIN

Written by mzalendoeditor

MABINGWA wa Ligi Kuu Tanzania bara Timu ya Yanga imetinga hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho barani Africa baada ya kuichapa bao 1-0 wenyeji  club Africain mchezo uliopigwa nchini Tunisia.

Shujaa wa Yanga ni kiungo mshambuliaji kutoka nchini Burkana faso akitokea benchi aliipatia bao muhimu timu yake dakika ya 79 Stephane Aziz Ki akimalizia pasi ya Fiston Mayele.

Kwa ushindi huo Tanzania imeingia hatua ya makundi timu mbili Simba SC wakiwa wametinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Africa

About the author

mzalendoeditor