WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
…………………………
Na Alex Sonna-DODOMA
Maafisa Maendeleo ya Jamii wametakiwa kujipanga kwenda na kasi ya Serikali ili kuchochea maendeleo ya jamii sambamba na sera, mikakati, sheria na miongozo mbalimbali wakati Serikali ikiendelea kufanyia kazi changamoto za upungufu wa watumishi, mazingira ya kazi na sheria ya taaluma hiyo nyeti.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ameyasema hayo akifungua kikao kazi cha Maafisa hao wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa jijini Dodoma Novemba 08, 2022 alipokuwa akifungua Mkutano wa Mwaka wa kada hiyo.
Dkt. Gwajima amesema, Serikali ina matumaini makubwa na mchango wa kada hii na itahakikisha inafanya uwezeshaji Ili kwenda na kasi iliyokusudiwa.
“Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan anatambua umuhimu wa sekta ya Maendeleo ya Jamii katika kuiwezesha Jamii kushiriki kujiletea maendeleo kwa kutumia rasilimali walizonazo hivyo kuwa kitovu cha maendeleo” na ndiyo maana amechukua hatua ya kuunda wizara mama ya sekta hii na mambo mengi mazuri yanakuja amesema Mhe. Dkt. Gwajima.
Akielezea umuhimu wa kada ya maendeleo ya jamii kwenye sekta zote amewapongeza kwa kazi nzuri wanayofanya katika kuwezesha mapambano ya kutokomeza ukatili wa kijinsia na kwa watoto huku akirejea mpango kazi wa Taifa wa kupambana na ukatili huo kwamba serikali inakamilisha ya utekelezaji wa miaka mitano iliyopita ili kuja na mpango mpya ambao utajibu mahitaji ya sasa kwenye mapambano haya.
Aidha amewapongeza Maafisa hao kwa kushirikiana na wanajamii hasa waliojitolea kupambana na vitendo vya ukatili na kuwahamasisha wananchi kushiriki shughuli za kiuchumi kupitia kampeni ya kijamii inayojulikana kwa jina la SMAUJATA hali inayochangia wananchi kuwa na uelewa na kutofumbia macho vitendo vya ukatili.
Mhe. Dkt. Gwajima amewakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii masuala yanayotekelezwa na Serikali na kwamba wakayasimamie ambayo ni majukwaa ya uwezeshaji wananchi kiuchumi, utekelezaji wa ahadi za nchi kupitia Jukwaa la kizazi chenye usawa ambapo Tanzani ni kinara wa eneo la haki na usawa wa kiuchumi, programu ya malezi na makuzi ya watoto kwa kutoa mafunzo ya malezi chanya kwa wazazi na walezi.
Mengine ni pamoja na utekelezaji wa Ajenda ya Kitaifa ya kuwekeza katika afya na maendeleo kwa vijana balehe, programu jumuishi ya malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto, usimamizi wa NGOs pamoja na uratibu wa machinga.
Wakati huo huo, Waziri Dkt. Gwajima amezindua mwongozo wa majadiliano wa mila na desturi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula amewataka Maafisa hao kutimiza majukumu yao kulingana na mipango iliyowekwa na sheria zilizopo “Maafisa Maendeleo ya Jamii, muda wa kuambiana umepita kila mmoja asimame vema Fanyeni kazi na Wadau. Kila mnachopanga Mpange na Wadau” amesema Dkt. Chaula.
Naye Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI Bw.Ramadhami Kailima,amesema kuwa Maafisa Maendeleo ya Jamii ndio Wasimamizi na Watekelezaji na amewahimiza watumie Mikutano ya Mkoa na Wilaya kuzungumzia Majukumu yao.
Awali Mkurugenzi shirika lisilo la Kiserikali la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini Yasin Ally amesema nchi haiwezi kufanikiwa bila kuwekeza kwenye Maendeleo ya Jamii.
Aidha amewahimiza Maafisa Maendeleo ya Jamii kuthibitisha uwepo wao kwenye maeneo yao ambapo ameiomba Ofisi ya Rais TAMISEMI kutoa Mwongozo wa Ulinzi na Usalama wa Mtoto na kuwepo Mpango kazi utaowezesha kukutana na Makundi Maalum.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizungumza wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Mwanaidi Ali Khamis,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
NAIBU Katibu Mkuu TAMISEMI Bw.Ramadhami Kailima,,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
Rais wa Chama cha Wataalam wa Maendeleo ya Jamii (CODEPATA) Angela Mvaa ,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
Mkurugenzi shirika lisilo la Kiserikali la kutetea haki za wanawake na watoto la Kivulini Yasin Ally,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
MWENYEKITI wa Bodi ya Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali nchini Mwantumu Mahiza,akizungumza wakati wa kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
SEHEMU ya washiriki wakifatilia hotuba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (hayupo pichani) wakati akifungua kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.
WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akizindua mwongozo wa majadiliano wa mila na desturi mara baada ya kufungua kikao kazi cha Maafisa wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Maendeleo ya Jamii wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kilichoanza leo Novemba 8,2022 jijini Dodoma.