Na Bolgas Odilo,Mzalendo blogs
YANGA imejiweka njia panda kutinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho barani Afrika baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na timu Club African mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Yanga Sc licha ya kulazimisha sare ya bila kufungana kwenye mchezo huo wameonesha kuhitaji ushindi kwa kucheza kandanda safi kwa kujitahidi kutafuta bao bila mafanikio .
Sasa Yanga inahitaji kwenda kushinda katika mchezo wa ugenini utakaochezwa nchini Tunisia Jumatano Novemba 9,mwaka huu au sare ya kufungana mabao ili aweze kufuzu hatua ya makundi.