Na Bolgas Odilo,Mzalendo Blogs
Mara baada ya kupoteza mchezo wao kwa bao moja kwa bila dhidi ya Azam FC Timu ya Simba hasira zote imeshushia Mtibwa Sugar kwa kuiadhibu mabao 5-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Kiungo Mkabaji Mzamiru Yassin alianza kuwanyanyua mashabiki wake mnamo dakika ya 38 na kuwapeleka mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 huku Mtibwa akiwa nusu baada ya mchezaji wake Kitenge kupewa kandi nyekundu.
Kimbunga cha mabao kiliongezeka katika kipindi cha pili Simba walipata mabao manne kupitia kwa Pape Sakho dakika ya 48 na 90,Augustine Okrah dakika ya 63 pamoja na Moses Phiri dakika ya 73 huku Mtibwa wakipata pigo lingine baada ya beki wake Cassian Ponela kuonyeshwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu.
Kwa ushindi huo Simba wameshusha Mtibwa nafasi ya pili wakiwa na pointi 17 huku Yanga wakiwa wanaongoza Ligi wakiwa na Pointi 20.