Featured Kitaifa

MRADI WA MAJI WA SH.BILIONI 1.6 KWENDA KUMALIZA CHANGAMOTO YA MAJI HIFADHI YA TAIFA RUAHA

Written by mzalendoeditor


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV- Ruaha

HIFADHI
ya Taifa ya Ruaha imesema kwa sasa kuna mradi mkubwa wa maji ambao
unaendelea katika eneo la Malumbe Kijiji cha Tungamalenga kwa lengo la
kuhakikisha maji hayo yanafika kwenye eneo la ndani ya hifadhi hiyo, ili
kuondokana na adha ya kukosa maji safi na salama.


Imeelezwa
kwamba ili kufanikisha mradi huo kiasi cha Sh.bilioni 1.6 kimepangwa
kutumika kuanzia mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika kwake na kwamba
ulianza Septemba na unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu na hivyo
kutaondoa adha ya kukosekana kwa maji safi na salama iliyoko kwa muda
mrefu.


Akizungumza
na waandishi wa habari Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya
Taifa ya Ruaha Godwell Ole Meing’ataki amesema kuwa kwa sasa
wanaendelea na ujenzi wa mradi mkubwa wa maji ambao unatekelekezwa kwa
ushirikiano wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha pamoja na wananchi wa
Tungamalenga na Msembe na maji hayo yatakwenda ndani ya hifadhi hiyo.


“Maji
haya yanaelekea katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha hasa eneo la Msembe
lakini pia maji haya yatapelekwa kwenye tenki lililopo Kingamalenga kwa
ajili ya jamii ya watu wa pale , ikumbwe kwamba Hifadhi ya Taifa ya
Ruaha kwa miaka 58 tangu ianze kumekuwa na changamoto kubwa ya maji na
maji yaliyokuwepo katika eneo hili hayana ubora na sio salama , mara
nyingi haya maji hayafai kwa ajili ya kupikia , kunywa kwani ni maji
ambayo yana chumvi chumvi hata ukijaribu kuoga hautakati hata ukitumia
sabuni maji haya hayafai.


“Na
pia viwango vya madini mbalimbali kwenye maji haya yako juu na sio
mazuri haishauri kwa binadamu kunywa wala kupikia.Hata ukitaka kupikia
utakuta sufuria inabadilika kutokana na chumvi nyingi, sasa Hifadhi yetu
ya Taifa ya Ruaha kwa kushirikiana na kijiji cha Kingamalenga walibuni
mradi huu na sasa utakwenda kuhakikisha uhakika wa maji safi na salama
yanapatikana katika kijiji cha Msembe kwa ajili ya matumizi ya watumishi
,familia zao lakini na idadi kubwa ya wageni ambao wanatembelea hifadhi
ya taifa ya Ruaha


“Huu
mradi umetoka hapa mpaka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha eneo la Msembe
takribabani kilometa 36, mitaramo na mabomba yameshatandazwa katika
kilometa hizo , kazi ambayo inafanyika hapa ni kujenga eneo la dakio la
maji na baada ya hapo tutaunganisha mabomba na kupeleka maji eneo la
Msembe.Pia tumejenga tenki kubwa kwa ajili ya kutunza haya maji halafu
tutakwenda kuyasambaza hadi hifadhini,”amesema.


Hivyo
amesema kwa hiyo mradi huo ni wa kipekee ambao unaonesha manufaa ya
ushirikiano kati ya wananchi wanaoishi jirani na hifadhi kwani bila ya
mahusiano mema kati yao na wananchi wasingeruhusiwa kuchukua maji ambayo
hata wao wananchi wanayahitaji.Pia wasingeruhusu mitaro na mabomba
kupita kwenye mashamba yao, maeneo ya makazi kwa ajili ya kupela maji
kwenye Hifadhi ya Taifa Ruaha.


“Tunashukuru
kwa ushirikiano ambao tumeupata na huu ni mradi mkubwa ambao unakwenda
kunufaisha hifadhi lakini na wananchi nao kwa upata maji safi na salama,
huu mradi ni mkubwa na umetumia takribani Sh.bilioni 1.6 ambazo ndio
zimetumika kwenye huu .Lakini kubwa zaidi katika kipindi cha kutekeleza
mradi wananchi hawa wamekuwa waaminifu.Tunachohurahia maji yapo ya
kutosha.


Kwa
upande wake Ofisa Uhifadhi wa Taifa Ruaha Kitengo cha Uhusiano kwa
Jamii Priscus Mrosso amesema hifadhi hiyo makao makuu yake yapo Msembe
ambacho ni kitongoji cha Kijiji cha Kingamalenga kwa hiyo wameuchukua
mradi huo katika Kijiji cha Malunde.“Ni sehemu ya ujirani mwema na ni
mradi ambao unakwenda kutunufaisha sisi wote.


“Kwa
awamu hii ambayo mradi unatekelezwa sasa hivi Tungamalenga watapata
maji kidogo lakini kwenye awamu ya pili ya mradi ambayo hayajatolewa la
maji lakini awamu ya pili watapata maji mengi , kwani tutaongezea nguvu
kwenye tanki lao kubwa la maji ambalo liko hapa kwenye kijiji. Mahusiano
kati ya hifadhi na kijiji cha Kingamalenga yako vizuri ndio maana
waliliridhia hifadhi kupitisha mabomba katika maeneo yao ya mashamba,
pia waliahidi mabomba hayo watayalinda kwani wanajua watanufaika na hayo
maji ambayo yanatakiwa kutoka Kijiji cha Malumbe mpaka
hifadhini,”amesema.


Wakati
huo huo Ofisa Mtendaji Kijiji cha Tungamalenga Linuss Mweluka amesema
mahusiano kati yao,TANAPA na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha hayajaanza leo ni
muda mrefu na wamekuwa wakipata wa kujengewa majengo mbalimbali taasisi
hasa Elimu na Afya .


“Lakini
kwa mradi huu wa maji tunasema umefika kwa wakati kwasababu kijiji
chetu kilikuwa na changamoto sana ya maji ya bomba , kwa mahusiano
tuliyonayo na TANAPA hadi sasa tumeshaambiwa tunaletewa maji hayo na
tutawekewa kwenye tenki ambalo lipo hapa kwa ajili ya kutumia sehemu
kubwa kwa taasisi mbili elimu na afya kwa awamu hii ya kwanza


“Kwa
awamu ya pili tutatoa maombi kwa ajili ya huduma kwa ujumla ya kijiji
kizima kwa hiyo kwa niaba ya wananchi na Serikali ya Kijiji cha
Kinamalenga napenda kutoa shukrani zangu za awali kwa TANAPA , ahadi
yetu sisi ni kutoa ushirikiano hasa katika ulinzi wa mradi kwasababu
mara nyingi kwenye miradi kama hii ya maji ambapo kumepita mabomba huwa
kunatokea uharibifu lakini tumejipanga ili kulinda vizuri mradi huo.”


Kuhusu
ushiriki wao kwenye kulinda hifadhi hiyo amesema kupitia elimu ambazo
zimekuwa zikitolewa wananchi wamekuwa na uelewa mkubwa kuhusu umuhimu wa
hifadhi na ndio maana hata ujangili kwa sasa umepungua.


Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Godwell Ole
Meing’ataki alipokuwa akizungumza mambo mbalimbali kuhusu hifadhi hiyo
ukiwemo mradi mkubwa wa maji ambao unaendelea katika eneo la Malumbe
Kijiji cha Tungamalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuhakikisha maji hayo
yanafika kwenye eneo la ndani ya hifadhi hiyo, Ambapo katika Mradi huo
kiasi cha Sh.bilioni 1.6 kimepangwa kutumika kuanzia mwanzo wa ujenzi
hadi kukamilika kwake na kwamba ulianza Septemba na unatarajia
kukamilika Desemba mwaka huu na hivyo kutaondoa adha ya kukosekana kwa
maji safi na salama iliyoko kwa muda mrefu.Kamishna
Msaidizi wa Uhifadhi,Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha Godwell Ole
Meing’ataki akiwa eneo unapojengwa mradi mkubwa wa maji ambao unaendelea
katika eneo la Malumbe Kijiji cha Tungamalenga mkoani Iringa kwa lengo
la kuhakikisha maji hayo yanafika kwenye eneo la ndani ya hifadhi hiyo,
Ambapo katika Mradi huo kiasi cha Sh.bilioni 1.6 kimepangwa kutumika
kuanzia mwanzo wa ujenzi hadi kukamilika kwake na kwamba ulianza
Septemba na unatarajia kukamilika Desemba mwaka huu na hivyo kutaondoa
adha ya kukosekana kwa maji safi na salama iliyoko kwa muda mrefu. PICHA
ZOTE NA MICHUZI JR-RUAHA.Ujenzi
wa mradi mkubwa wa maji ambao unaendelea katika eneo la Malumbe Kijiji
cha Tungamalenga mkoani Iringa kwa lengo la kuhakikisha maji hayo
yanafika kwenye eneo la ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruahahiyo
kuondokana na adha ya kukosa maji safi na salama.


Mmoja
wa wakazi wa Kijiji cha Tungamalenga ambaye pia mmoja wa mafundi
wanaoshiriki kwenye ujenzi wa Mradi huo akieleza manufaa makubwa
watakayoyapata mara baada ya kukamilika kwa mradi huo,ambao pia
utanufaisha vijiji vya jiraniOfisa
Uhifadhi wa Taifa Ruaha Kitengo cha Uhusiano kwa Jamii Priscus Mrosso
akizungumza na Ofisa Mtendaji Kijiji cha Tungamalenga Linuss Mweluka
kuhusu kuendelea kuimarisha mahusiano yao ya ujirani mwema kati
yao,TANAPA na Hifadhi ya Taifa ya Ruaha,lakini pia kuhakikisha
wanashiriki kulinda miradi mbalimbali inayoratibiwa na Hifadhi ikiwemo
Elimu na Afya.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUAHA.

About the author

mzalendoeditor