Na. Mwandishi wetu
Ni muendelezo wa mapinduzi ya kukata kiu ya wananchi na hatua kwa hatua kusapoti maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ya kumtua mama ndoo kichwani Dawasa wameamua kufanya Kwa vitendo.
Wananchi maeneo ya Kisanga,Kilimahewa,Muungano,Kinzudi,Majengo,Salasala,Muungano na Mivumoni waipongeza DAWASA kwa kuwasogeza huduma ya maji karibu baada kupokea vifaa vya kuunganishiwa maji katika Mkoa wa Kihuduma DAWASA Mivumoni.
Ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa Mradi wa Uboreshaji wa huduma ya Maji kutoka Bagamoyo hadi Makongo unaotarajiwa kukamilika Disemba 2022.
Dhumuni kubwa la Mradi huo ikiwa ni kujidhatiti katika kuboresha huduma ya maji na kufikia wananchi Kwa asilimia 95 kwa wateja wapya ambao hawajawahi kupata huduma ya Maji safi na salama hapo awali.
‘Tunapaswa kuwapongeza na kuwapa hamasa watendaji wakuu wa DAWASA akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA kwa kazi kubwa wanayofanya katika kuunganisha na kuboresha miundombinu ya maji safi na salama Kwa wananchi wa Dar na PWANI’ Walisema baadhi ya wananchi walioguswa na huduma hiyo.