Featured Kitaifa

WADAU WATOA MAONI YAO JUU YA MISWADA MINNE YA SHERIA

Written by mzalendoeditor

 

Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Dk. Fredrick Shoo akitoa maoni yake kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Jamii Forums Tanzania Ndg. Maxence Mero  akiwasilisha maoni ya Taasisi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo. 

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria wakipokea maoni ya wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria mbalimbali Namba 3 wa Mwaka 2022.

Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakijadili maoni ya Wadau kuhusu Muswada wa Sheria ya Uwekezaji ya mwaka 2022.

Wadau mbalimbali wakishiriki kutoa maoni yao kuhusu Muswada wa Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo.

Mwakilishi wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania Ndg. Paul Kisabo akiwasilisha maoni kuhusu Muswada wa Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi wa Mwaka 2022 mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu katika ukumbi wa Msekwa Bungeni hii leo. (Picha na Ofisi ya Bunge)

 

About the author

mzalendoeditor