Featured Michezo

TAMISEMI QUEENS TIMU YA KUVUTA KAMBA YAANZA KWA MOTO  SHIMIWI

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, Tanga

Tamisemi Queens wameanza vizuri mechi yao ya mchezo wa kuvuta kamba kwa kuwashinda pointi 2-0 Wizara ya Mambo ya Nje katika mshindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali Tanzania (SHIMIWI) yanayoendelea Jijini Tanga.

Mechi hiyo iliyochezwa leo mapema asubuhi katika viwanja vya Shule ya Sekondari Usagara Jijini Tanga, kwa timu zote kuonekana na utayari wa mchezo huo kwa kuonesha uwezo wa kuvutana kwa sekunde za mwanzoni na baadaae Tamisemi Queens kuzidisha uwezo zaidi wa kuvuta kamba na kuwashinda wapinzani wao pointi 2-0.

Tamisemi Queens mchezo wa kuvuta kamba kwa hatua ya makundi wamepangwa kucheza na timu ya MSD, Katiba na Sheria, Ras Shinyaga na Wizara ya Mambo ya Nje.Kwa upande wa Kocha wa Timu ya Tamisemi kuvuta kamba Chidiel Masinga amesema, hatua hiyo ya awali ambayo ni ya makundi wameanza vizuri na wapinzani wao Wizara ya Mambo ya Nje na wanategemea kufanya vizuri zaidi.

Chidiel amewaomba mshabiki wao na uongozi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kuendelea kushirikiana nao na kuwaombea ili waendelee kufanya vizuri zaidi sababu wachezaji wanabidii, wanajituma, wananidhamu na wanaelewa kwa kile wanachoelekezwa kutoka kwa viongozi wao.

Naye Kapteni wa Timu ya Kamba Saida Marijani ameshukuru viongozi kwa kuendelea kuwafundisha kwa bidii na uongozi wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI kwa kuiruhusu timu hiyo kuendelea kushiriki mashindano hayo na kuahidi wataendelea kujituma kwa kufanya vizuri zaidi.

About the author

mzalendoeditor