Featured Kitaifa

WAZIRI JAFO ATOA WIKI TATU WAFUGAJI KUONDOA MIFUGO KATIKA BONDE LA IHEFU

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe.Dkt Selemani Jafo akitoa maagizo ya kuondolewa kwa mifugo katika bonde la Ihefu

 

 

 Fredy Mgunda, Mbeya

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais- Muungano na Mazingira Mhe.Dkt Selemani Jafo ametoa wiki tatu kwa wafugaji wa Ng’ombe waliopo bonde na Ihefu kuondoa mifugo yao kutokana na uharibifu wa vyanzo vya maji vilivyopo katika hifadhi hiyo.

 

Dkt Jafo alisema kuwa wafugaji hao wamevamie bonde hilo ambalo lipo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha na kusababisha uharibu mkubwa wa hifadhi hiyo na vyanzo vya maji kuanza kupotea hivyo wanatakiwa kuondoka ndani ya wiki tatu.

 

Alisema kuwa watakapokutana mawaziri watatoa maamuzi magumu ambayo wafugaji hawatayapenda hivyo ni bora waondoke mapema kabla ya zoezi hilo kuwakuta na kuwaletea madhara hivyo watumie uhuru wao wa sasa kuondoa mifugo katika bonde hilo.

 

 Dkt  Jafo alisema kuwa mifugo hiyo imekuwa mingi kiasi kwamba imeanza kuharibu vyanzo vya maji vilivyopo katika bonde hilo la Ihefu hivyo serikali isipodhibiti basi maji yatapotea na huduma nyingine za maji nazo zitaathirika.

 

 

Alisema kuwa maji yanayotoka katika bonde la Ihefu yanachangia katika bwawa la kufua umeme la mwalimu Nyerere na wanyama waliopo katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha wanategemea maji hayo pia hivyo ni muhimu kutunza vyanzo hivyo.

 

“Kwa mujibu wa sheria za mazingira  natoa wiki tatu wenyw mifugo yao waondoe mifugo yao kwa hiyari yak wakati oparesheni ikiendelea katika bonde la Ihefu la sivyo sheria ya kulinda vyanzo vya maji itachukua mkondo wake” alisema Dkt Jafo

 

Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera alisema kuwa Ng’ombe ni wengi kuliko wanyama katika hifadhi ya Taifa Ruaha kwenye bonde la Ihefu hiyo inatoka na wanyama wengi kukimbia madhara yanayotokana na Ng’ombe hao.

 

“Tumetembea angani na umeona mwenyewe namna gani ambavyo wafugaji hao wanavyoharibu vyanzo vya maji na uharibifu unaoendelea katika hifadhi ya Taifa ya Ruaha”alisema RC Homera

About the author

mzalendoeditor