Featured Michezo

DJUMA,MAYELE,AZIZ KI WAING’ARISHA YANGA DHIDI YA MTIBWA SUGAR

Written by mzalendoeditor

Na Eva Godwin,MZALENDO BLOG

MABINGWA Watetezi Yanga SC wamendelea kutunza rekodi yao ya kucheza mechi 41 bila kufungwa mechi za Ligi baada ya kuichapa  mabao 3-0 Mtibwa Sugar katika mechi ya Ligi Kuu Tanzania bara mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Yanga walipata bao mawili kipindi cha kwanza yakifungwa na Djuma Shaban dakika ya 33 na Mshambuliaji hatari kwa sasa katika Ligi Kuu Fiston Mayele dakika 38.

Kipindi cha pili Yanga walipata bao la tatu likifungwa na Stephanie Aziz Ki dakika ya 91 likiwa bao lake la kwanza tangu ajiunge na Yanga.

Kwa Ushindi huo Yanga wamepanda mpaka nafasi ya kwanza ya msimamo wa Ligi Kuu wakifikisha pointi 10 wakiwa wamecheza mechi nne,nafasi ya pili ikishikwa na Azam FC ambao wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City leo na kufikisha Pointi 8.

Wekundu wa Msimbazi Simba wakiwa na Pointi zao 7 wakiwa nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza  mechi tatu kesho watashuka katika uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kucheza na Tanzania Prisons.

About the author

mzalendoeditor