Uncategorized

PROF.SHEMDOE AZITAKA HALMASHAURI NCHINI KUBUNI VYANZO VYA MAPATO

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof.Riziki Shemdoe,akizungumza kwenye mkutano wa Programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma (PIC) kilichojumuisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wataalamu wa utekelezaji wa program hiyo na wadau kutoka Uingereza, Canada na Norway uliofanyika loe Februari 25,2022 jijini Dodoma.

 Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI  Dkt. Switbert Mkama,akizungumza katika  mkutano wa Programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma (PIC) kilichojumuisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wataalamu wa utekelezaji wa program hiyo na wadau kutoka Uingereza, Canada na Norway uliofanyika loe Februari 25,2022 jijini Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Masuala ya Kisiasa na Kiutawala Ubalozi wa Uingereza Saurence Wilkes,akizungumza wakati wa Mkutano wa Programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma (PIC) kilichojumuisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wataalamu wa utekelezaji wa program hiyo na wadau kutoka Uingereza, Canada na Norway uliofanyika loe Februari 25,2022 jijini Dodoma.

WASHIRIKI wakifatilia hotuba mbalimbali wakati wa Mkutano wa Programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma (PIC) kilichojumuisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wataalamu wa utekelezaji wa program hiyo na wadau kutoka Uingereza, Canada na Norway uliofanyika loe Februari 25,2022 jijini Dodoma.

…………………………………………………………

Na.Alex Sonna,DODOMA

KATIBU Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Prof.Riziki Shemdoe,amezitaka Halmashauri nchini kubuni vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo haviumizi wananchi ili zijitegemee.

Prof.Shemdoe ameyasema hayo leo Februari 25,2022 jijini Dodoma wakati wa Mkutano wa Programu ya maboresho ya usimamizi wa fedha za umma (PIC) kilichojumuisha Makatibu Tawala wa Mikoa, Wataalamu wa utekelezaji wa program hiyo na wadau kutoka Uingereza, Canada na Norway.

Prof.Shemdoe amesema katika programu ijayo tuweze kusaidia kuongezeka kwa vyanzo vya mapato ili kuondokana na hali ya sasa ya kupandisha kwenye chanzo hicho.

‘Katika programu ijayo iweze kusaidia kwenye kuongezeka kwa vyanzo vya mapato ili kuondokana na hali ya sasa ya kupandisha kwenye chanzo hicho hicho badala ya kuwa na vyanzo vingi ambavyo havitaumiza wananchi.’amesema Prof.Shemdoe

Hata hivyo, Prof.Shemdoe amesema kuwa katika kumaliza program hiyo hadi sasa uwezo wa kujitegemea wa Halmashauri nchini ni kwa asilimia 15 huku zikitegemea serikali kuu kwa asilimia 85.

“Kwa mradi huu na kwa namna tulivyokuwa tunafanya kazi tukiendelea na program hii ya maboresho tutafika mahali Mamlaka zetu zitajitegemea zenyewe, Majiji yamekuwa na uwezo mkubwa zaidi yah ii asilimia 15 hii tumechukua kwa halmashauri zote,”amesema Prof.Shemdoe

Prof. Shemdoe amesema matumizi ya fedha nje ya bajeti kwa halmashauri nchini umepungua kutoka asilimia 10 mwaka 2016/17 hadi kufikia asilimia 2 mwaka 2020/21.

Ameongeza kuwa upelekaji wa fedha zilizotengwa kwenye bajeti kutoka Serikali Kuu kwenda Mamlaka ya Serikali za Mitaa yameongezeka kutoka asilimia 60 mwaka 2016/17 hadi kufikia asilimia 85 mwaka 2020/21.

Prof. Shemdoe amesema kumekuwapo na kupungua kwa hoja za ukaguzi sambamba na kuongezeka kwa uwazi kwenye manunuzi.

‘Mkakati uliopo ni kuzungumza na wadau kuangalia namna ya kuja na programu hii awamu ya sita ambapo mambo kadhaa yataingizwa ikiwamo ya kukabiliana na changamoto ya matumizi ya fedha mbichi’ amesema Prof.Shemdoe

Kwa upande wake Mratibu wa programu hiyo, Lucas Mrema amesema programu hiyo imeweza kusaidia kuimarisha mfumo funganishi wa usimamizi na udhibiti wa matumizi ya fedha ambao umefungwa katika halmashauri 185.

”Lengo la programu hiyo ni kuimarisha mifumo ya usimamizi wa fedha za umma kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa.”amesema Mrema

About the author

mzalendoeditor