Featured Kitaifa

SERIKALI KUENDELEA KUWALINDA WANANCHI KUTOKANA NA UHALIFU WA MITANDAONI

Written by mzalendoeditor

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akizungumza wakati akifunga mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifunga mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Camilius Wambura,akitoa maelezo kuhusu waliyojifunza wakati wa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

Mkurugenzi wa TEHAMA kutoka Wizara ya Habari,Mawasiliano na Teknolojia ya Habari ,akizungumza wakati wa kufungwa kwa mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Joshua Mwangasa ,akizungumza wakati wa kufungwa kwa  mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

WASIRIKI wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi (hayupo pichani),wakati akifunga mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akikabidhi vyeti kwa baadhi ya washiriki mara baada ya kufunga  mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

……………………………………………………….

Na.Alex Sonna,DODOMA

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dk.Jim Yonazi,amesema kuwa Serikali itaendelea kuwalinda wananchi wake kutokana na uhalifu wa mitandaoni.

Hayo ameyasema  jijini Dodoma wakati akifunga mafunzo ya makosa ya mtandao kwa wapelelezi na askari wa chumba cha mashtaka wa Jeshi la Polisi Tanzania yaliyoamalizika leo Februari 25,2022  Jijini Dodoma.

Dk.Yonazi amesema kuwa bado kuna kazi kubwa ya kukabiliana na uhalifu huo kwa kuwa kila siku zinaibuka mbinu mpya za kihalifu.

“Mafunzo haya ni muhimu kwa usalama wa nchi, Wizara inaendelea kutenga fedha za kuhakikisha nchi ipo salama,”amesema Dk.Yonazi

Amesema kuwa watumiaji wa huduma ya mtandao (internet) idadi ni kubwa ambayo hivyo ni muhimu sana kuweka namna sahihi ya kulinda usalama wake.

“Katika kujenga uwezo wa nchi mzigo wa usalama wa nchi tumetwishwa sisi tulio hapa, tunajukumu kubwa sana kuhakikisha kwamba tunalinda usalama wa nchi yetu kupitia uwezo tuliojengewa.”amefafanua

Amesema, kupitia mafunzo hayo ya siku tano,walinzi hao wa usalama mtandaoni wanapaswa kushirikiana katika hatua changamoto zote uhalifu mtandao na kwamba Kwa kufanya hivyo watadhihirisha namna ambavyo Tanzania imejipanga katika kuhakikisha matumizi ya mitandao yanakuwa salama.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Camilius Wambura,amesema kuwa idara hiyo itahakikisha inaboresha mifumo ya kuhakiki uhalali wa taarifa zinazopitia kwenye mitandao ambayo imebuniwa na wataalam wa Teknolojia ya Habari nchini ili kuzuia matumizi mabaya ya mitandao.

“Makosa ya mtandao yanakuwa mengi na kusababisha uvunjifu wa amani na kuharibu furaha Kwa watu wengine,kupitia mafunzo hayo yataleta matokeo chanya kutokana na mbinu mlizopata ili kukabiliana na uhalifu wa kimtandao kwani maarifa yatawasaidia katika kubadilishana taarifa,”Amesema.

Hata Wambura amewataka  wapelelezi hao pamoja na askari kuhakikisha wanazingatia misingi ya kazi na wito wa maadili ya kazi yao ikiwa ni pamoja na kufanya kazi kwa kushirikiana ili kuweza kufikia malengo.

About the author

mzalendoeditor