Na Eva Godwin-DODOMA
SERIKALI imeanza kutekeleza Mradi wa Maji Wenye Thamani zaidi ya Shilingi Bililioni 100 huku Wananchi zaidi ya Laki Nne Wakitarajiwa kunufaika na Utekelezaji wa mradi huo kutoka ziwa Victoria kwenda Wilaya ya Rorya hadi Tarime Vijijini.
Ameyasema hayo Waziri wa Maji Juma Aweso katika hafla ya utiaji saini baina ya Wakandarasi Leo 1 Septemba, 2022 Jijini Dodoma.
Amesema Changamoto kubwa iliyojitokeza ilikuwa ya utekelezaji wa Mradi huo ambao umekuwa wa Muda mrefu.
“Mradi huu utagharimu shilingi bilioni 134 na shilingi Milioni 398 ambazo ni fedha nyingi za walipa kodi na hii ni kuokoa uhai wa Wananchi wa Rorya na Tarime na ni mradi ambao utatekelezwa kwa miezi thelathini
” Jukumu letu lililobaki ni moja la kumtafuta mkandarasi mwenye uwezo wa kufanya kazi hii na mwenye uzoefu na imani yetu atajenga kwa wakati uliopangwa hili kuhakikisha mradi huu unakamilika na Wananchi wanapata Maji safi na Salama”. Amesema Aweso
Ameongezea kwa kusema Mradi huo ukikamilika Watanufaika Watu zaidi ya laki4 na 60 na 85% ya Maji Vijini utakamilika na 90% Ya Maji Mjini utakamilika
Na pia amewaomba Wabunge pamoja na viongozi wote wa Tarime na Rorya kuwa na ushirikiano na kama watakuwa na changamoto zozote waijulishe Wizara ila mradi utekelezwa kama ilivyopangwa.
Aidha Katibu Mkuu Wizara ya Maji Injinia Anthony Sanga amesema kuwa Wasimamizi wa mradi wanapaswa kupata maoni ya wabunge na kuwepo katika eneo la chanzo ili kusimamia nradi huo kwa kutatua changamoto kwa huaraka zaidi.
” Mradi huu unahitaji ufuatiliaji mkubwa hili kuweza kutatua changamoto kwa huaraka ambazo zitajitokeza kwa wakati huo na hii itasaidia kukamilika kwa mradi mapema
Niwaombe tu Wabunge pamoja na viongozi wa juu wa Jimbo la Tarime Vijijini kuwa na ushirikiano kuhakikisha mradi huu mnausimamia najua Wakandarasi wetu niwataalamu na wazoefu wa muda mrefu katika suala la ujenzi”. Amesema Sanga
Naye Mbunge wa Jimbo la Tarime Vijijini
Mwita Waitara amesema Mradi huo ukifika Tarime uchumi utapanda sana utakuwa ni ukombozi wa almashauri ya Tarume huku akiomba Mradi huo huanze maeneo ya tarume mjini na kuelekea Vijijini,
“Mradi huu utakuwa ni ukombozi kwa Almashauri ya Tarime, na tunaomba mradi huu ukifika chanzo kianze Tarime mjini kuanzia Maeneo ya Sirali, Nyamwaga mpaka Nyamongo
“Na ikiwapendeza Mhe.Waziri Wataalamu wakaweka dizaini ya Maji hayo yakiwa yanaenda Tarime yashuke na Nyamongo kwasababu nyamongo kuna chanzo cha maji machafu ili chanzo hicho cha Maji machafu yaondolewe na kubaki Maji Masafi hii itasaidia sana”. Amesema Waitara
Mbunge Jimbo la Rorya Jafari Chenge amesema Jimbo lake la Rorya asilimia 77% limezungukwa na Maji na haukuwa na mradi mkubwa zaidi ya bilioni 1 ambapo unatokana na ziwa victoria.
“Wananchi wa Rorya wameteseka kwa muda mrefu sana katika suala hili la upatikanaji wa Maji, ila tumeona Wizara ya Maji ikifanya Jitihada kutatua changamoto hii kupitia vyanzo mbalimbali na haikuwa kazi rahisi kwao kutatua changamoto hii” .Amesema Chenge