WATU wawili wanashikiliwa na Jeshi la polisi mkoani Kigoma kwa tuhuma za mauaji ya mwanamke aitwaye Lidya Kamala na kisha kumpora fedha kiasi cha Sh.Milioni 9.5 alizokuwa amekwenda kuzifanyia zindiko la biashara kwa Mganga wa kienyeji.
Watu hao wanaoshikiliwa ni Dereva wa pikipiki na Mganga wa kienyeji ambao wanadaiwa walifanya mauaji hayo kwa kushirikiana na kisha kufukia mwili wake.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, James Manyama, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amedai kuwa Lidya alikuwa ameenda kuzindika fedha za biashara kwa mganga huyo kiasi cha sh. milioni 9.5 lakini watuhumiwa hao walipora fedha hizo na kumuua.