MKUU wa Dodoma Rosemary Senyamule akizungumza na Karani wa Sensa Bi.Theresia Sagamilwa wakati alipokuwa akihesabiwa nyumbani kwake Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 23 Agosti 2022 kwenye Shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
………………………………..
Na Alex Sonna-DODOMA
MKUU wa Dodoma Rosemary Senyamule ,amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la sensa kwa kutoa taarifa sahihi
RC Senyamule ameyasema hayo nyumbani kwake uzunguni jijini Dodoma mara baada ya kuhesabiwa wakati wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi lililoanza rasmi leo tarehe 23 Agosti 2022, nchini kote.
Mhe. Senyamule ametoa rai kwa wakazi wote wa mkoa wa Dodoma kutoa ushirikiano kwa makarani wa sensa ili waweze kupata taarifa sahihi zitakazowezesha serikali kupanga vema maendeleo.
Amesema kuwa maswali yanayoulizwa na makarani wa sensa ni rahisi na mtu yoyote anaweza kuyajibu hivyo wananchi wasiwe na wasiwasi na wasiogope kwenye kushiriki zoezi hilo.
”Nimefurahishwa na maswali yanayoulizwa katika zoezi la sensa ya watu na makazi ambayo yanalenga huduma muhimu za kijamii zinazopatikana katika maeneo ya wananchi ili kuiwezesha serikali kutambua huduma zinazokosekana katika maeneo hayo na uhitaji wake.”amesema RC Senyamule
Aidha Mhe. Rosemary Sitaki Senyamule amesema kuwa zoezi hilo baada ya kuzinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan linaendelea vizuri katika mkoa huo na hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza katika zoezi hilo.
“Zoezi la sensa limezinduliwa na mhe Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Agosti 23,2022 na litaendelea kwa siku saba na mpaka sasa hakuna changamoto yoyote iliyojitokeza hapa Dodoma na hivyo linaendelea vizuri”
MKUU wa Dodoma Rosemary Senyamule akizungumza na Karani wa Sensa Bi.Theresia Sagamilwa wakati alipokuwa akihesabiwa nyumbani kwake Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 23 Agosti 2022 kwenye Shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi .
MKUU wa Dodoma Rosemary Senyamule,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhesabiwa nyumbani kwake Uzunguni jijini Dodoma leo tarehe 23 Agosti 2022 kwenye Shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi