Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Karani wa Sensa Phausta Ntigiti wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 kwenye shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waandishi wa Habari mara baada ya kuhesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
KAMISAA wa Sensa ya Watu na Makazi Tanzania bara Anna Makinda,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuhesabiwa katika Makazi yake Chamwino Ikulu Mkoani Dodoma tarehe 23 Agosti, 2022 katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi, wakimsikiliza Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Bi.Asia Hassan Mussa wakati wa zoezi la kuhesabiwa lililofanyika katika makaazi yake Migombani Ikulu Ndogo leo 23-8-2022, zoezi hilo la Sensa ya Watu na Makazi lilioza leo kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango pamoja na Mkewe Mama Mbonimpaye Mpango wakizungumza na Karani wa Sensa Isack Mgosho wakati walipokuwa wakihesabiwa katika Makazi yao Chanika Jijini Dar es salaam leo tarehe 23 Agosti 2022 kwenye Shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi .
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akihojiwa na kutoa majibu ya dodoso kuu la Sensa ya Watu na Makazi kwa Karani wa Sensa Amina Mwambe wakati alipokuwa akihesabiwa katika Makazi yake ya Kijiji cha Nandagala, Ruangwa Mkoani Lindi Agosti 23, 2022 wakati wa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Tulia Ackson ,akishiriki zoezi la sensa ya watu na makazi ambapo amehesabiwa katika makazi yake yaliyopo mtaa wa Sisimba, Uzunguni Jijini Mbeya.
MBUNGE wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu,akihesabiwa na Karani nyumbani kwake kata ya Ikungi.
Katibu wa Nec, Idara ya Organaizesheni Dkt. Maudline Cyrus Castico,akihesabiwa na Karani wa Sensa Bi, Ummy Abdalah katika makazi yake Kiembe Samaki Zanzibar.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) (kulia) na mkewe Bi. Neema Mwigulu Lameck Nchemba, wakihesabiwa na Karani wa Sensa Bi. Rosemary Shani, katika zoezi la Sensa ya watu na Makazi, kijijini kwao Misigiri Kiomboi Iramba Mkoani Singida .
Waziri wa Madini Dkt. Doto Biteko akijibu maswali aliyoulizwa na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Magera Kilosa wakati akihesabiwa nyumbani kwake Kata ya Bulangwa Wilaya ya Bukombe, Mkoani Geita.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt. Selemani Jafo akizungumza na Karani wa Sensa Bw. Jumanne Marko wakati alipokuwa akishiriki Sensa ya Watu na Makazi katika makazi yake katika Kitongoji cha Kimani wilayani Kisarawe mkoani Pwani leo Agosti 23, 2022 ambapo alitoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwa kutoa taarifa sahihi.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja akihojiwa na Karani wa Sensa, Anthony Mlegi (kulia), wakati akihesabiwa katika makazi yake kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi Wilaya ya Magu Mkoani Mwanza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu Mhe. George Simbachawene akiwa anatoa taarifa muhimu kwa Makarani wa Sensa ya Watu na Makazi nyumbani kwake Kibakwe Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Innocent Bashungwa akizungumza na Karani wa Sensa ya Watu na Makazi Spencia Rutalemwa wakati akihesabiwa nyumbani kwake kijiji cha Ahakishaka, Kata ya Nyabiyonza, wilaya ya Karagwe, Mkoani Kagera.