Na Odilo Bolgas
MABINGWA Yanga wameendelea kugawa dozi ugenini baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0 mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliochezwa uwanja wa Shekhe Amri Abeid jijini Arusha.
Yanga walipata bao dakika ya 4 likifungwa na Bernard Morrison akimalizia pasi ya Jesus Moloko bao hilo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko Yanga waliendelea kuutawala mchezo na mnamo katika dakika ya 67 Mshambuliaji hatari kutoka DRC Congo Fiston Mayele alipigilia msumari wa pili akimalizia krosi ya Shaban Djuma na kufunga kwa kichwa.
Mchezo mwingine umepigwa katika uwanja wa Liti Mjini Singida wenyeji Dodoma jiji wameendelea kugawa pointi baada ya kuchapwa mabao 2-1 dhidi ya Tanzania Prisons.
Mabao ya Prisons yamefungwa na Ismail Mgunda kwa mkwaju wa Penalti dakika ya 1 na bao la pili limefungwa na Jeremiah Juma huku bao la Kufutia machozi la Dodoma jiji limefungwa na hassan Mwaterema dakika ya 14 hii ni mechi ya pili kwa Dodoma ikizidi kupoteza baada ya kuchwa mabao 3-1 dhidi ya Mbeya City.
Mechi nyingine itachezwa katika uwanja wa Benjamin Mkapa majira ya saa moja usiku Wekundu wa Msimbazi Simba watacheza na Kagera Sugar kutoka Mkoani Kagera.