Featured Michezo

DAR ES SALAAM YAANZA VYEMA MPIRA WA KIKAPU NA WAVU UMISSETA

Written by mzalendoeditor

 

Asila Twaha- TABORA

Timu ya Dar es Salaam kwa upande wa wanaume mpira wakikakapu leo Agosti 11, 2022 wameanza vizuri kwa kuwafunga goli 66 wapinzani wao Arusha mechi iliyochezwa majira saa mbili asubuhi katika viwanja vya Tabora Wavulana.

Timu ya Dar es Salaam imeonekana ikicheza kwa umahiri kwa staili ya kuwapiga chenga nyingi timu ya Arusha na kuweza kufanya vizuri wakati wote.

Mashabiki wa mchezo upande wa Dar es Salaam wameonekana wakiwa na nyuso za furaha na bashasha kwa timu yao na kuwapa nguvu kwa kuwashangilia pale walipokuwa wanafunga na kwa upande wa timu Arusha kuzidiwa chenga na kuruhusu goli 66 kutumbukizwa katika upande wao na Arusha kuambulia goli 23.

Kwa wakati mwengine kwa upande mpira wa wavu wasichana Dar es Salaam wameichapa seti 3 Kilimanjaro kupata seti 1 na kuifanya Dar es Salaam kuanza vizuri kwa asubuhi ya leo wasichana wakisema mapambano yameanza na yanaendelea kwa kuutafuta ushindi.

Kwa upande wa mratibu mpira wa wavu Somo Kimwaga amesema, timu zote zipo vizuri na timu ya Dar es salaam kuonekana kuanza vizuri asubuhi ya leo ni uandaliwaji wa watoto katika kufanya mazoezi ameshauri ndio mechi zimeanza na watoto wote wanafanya vizuri kwa kucheza ameshauri walimu, viongozi kuendelea kuwapa ushirikiano watoto katika michezo yao ili wafanye vizuri zaidi.

About the author

mzalendoeditor