Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (Kulia) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Benki Kuu Tanzania tawi la Mbeya Bw Ibrahimu Malogoi alipotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki ya NBC inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (kulia) akibadilishana mawazo na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (kulia) akibadilishana mawazo na wadau wa kilimo waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Maofisa wa benki ya NBC wakitoa ufafanuzi kuhusu huduma zinazotolewa na benki hiyo kwa wadau mbalimbali waliotembelea banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
Timu ya maofisa wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi wa Wateja wadogo wa Benki ya NBC, Elibariki Masuke (wa tano kulia), Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa (wa tano kushoto) na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Mbeya Bi Asia Mselemu (wan ne kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja kwenye banda la maonesho ya kilimo la benki hiyo inayoshiriki Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya.
……………………………….
Na Mwandishi Wetu-Mbeya
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeendelea kung’ara kwenye Maonesho ya Kilimo Nanenane yanayofanyika katika Uwanja wa John Mwakangale mkoani Mbeya, huku huduma ya Bima ya Kilimo inayotolewa na benki hiyo kwa wakulima ikiwa ni moja ya vivutio vikubwa miongoni mwa washiriki wanaotembelea maonesho hayo.
Akizungumza kwenye maonesho hayo yaliyozinduliwa jana na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mkuu wa kitengo cha wateja wadogo wadogo, Lariba na wakulima kutoka Benki ya NBC, Bw Raymond Urassa alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye maonesho hayo ni muendelezo wa jitihada zake za kuendelea kujiweka karibu zaidi na wadau wa sekta hiyo muhimu.
“Kupitia Maonesho haya tunapata fursa ya kutangaza huduma zetu zinazohusiana na sekta nzima ya kilimo pamoja na kupokea mrejesho wa huduma hizo kutoka kwa wakulima.’’
Alisema ushiriki wa benki hiyo kwenye sekta ya kilimo unahusisha mkakati mkubwa wa benki hiyo unaolenga kuinua sekta ya kilimo nchini unaofahamika kama ‘NBC Shambani’ unaohusisha mnyororo wote wa sekta ya kilimo kuanzia kwa mkulima, mchakataji wa mazao ya kilimo hadi msambazaji.
“Zaidi pia tunalenga kuhakikisha tunashirikiana vema na serikali katika kutimiza adhma ya msingi kabisa ya kuhakikisha tunaongeza kwa kasi ukuaji wa sekta ya kilimo nchini ikiwa ni sambamba na kuboresha maisha ya wakulima wenyewe,’’ alibainisha.
Akizungumzia baadhi ya huduma zinazotolewa na benki hiyo mahususi kwa wakulima Bw Urassa aliitaja huduma ya Bima kwa wakulima inayotolewa na benki hiyo kwa kushirikiana na kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance inayolenga kuwalinda wakulima, wavuvi na wafugaji nchini dhidi ya hasara pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayoweza kuathiri uzalishaji wao.
“Benki ya NBC tuinatambua vema sekta ya kilimo na zaidi tunatambua mchango wa wa wakulima katika uchangiaji wa uchumi wa nchi na kwa msingi huu tumeona ni vema kuja na Bima ya mazao kwa wakulima. Katika kuthibitisha ufanisi wa huduma hii, ni hivi karibuni tu kwa kushirikiana na wenzetu kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance tuliwafidia wakulima wa tumbaku mkoani Tabora ambao mazao yao yaliathiriwa na hali ya hewa,’’ alibainisha.
Zaidi, aliongeza kuwa benki hiyo pia inawawezesha wakulima kwa kuwapatia pembejeo za kilimo kwenye baadhi ya mazao hususani yale ya kimkakati ikiwemo pamba, kahawa na tumbaku lengo likiwa ni kuongeza tija kwenye sekta hiyo muhimu.
“Kupitia mpango wetu wa NBC Shambani tumekuwa tukishirikiana na wadau mbalimbali katika kutoa mikopo mbalimbali kwa wakulima ikiwemo ya zana mbalimbali za kilimo ikiwemo matrekta na mashine nyingine nyingi,’’ alitaja huku akiwaomba wadau mbalimbali wa kilimo waliohudhuria maonesho hayo kutembelea banda la benki hiyo ili kupata ufafanuzi na huduma mbalimbali zinazohusiana na sekta hiyo.