Featured Kitaifa

MTAA WA HAMVU KATA YA CHANG’OMBE WAILILIA SERIKALI UBOVU WA BARABARA

Written by mzalendoeditor

MUONEKANO wa Barabara ya Mtaa wa Hamvu Kata ya Chang’ombe jijini Dodoma¬†

…………………..

Na Eva Godwin-DODOMA

MJUMBE wa Serikali ya Hamvu kata ya Chang’ombe Mkoani Dodoma ,Latifa Yusufu ameiomba Serikali Kutatuliwa changamoto ya Barabara inayowakabili Katika kata hiyo hasa katika kipindi cha kuelekea msimu wa Mvua ili kuepuka madhara yanayotokea kipindi cha Mvua nyingi.

Akizungumza na Mzalendo blog Agosti 2,2022 katika ofisi za Mwenyekiti wa mtaa Jijini Dodoma

Amesema ni takribani miaka minne (4) sasa tangu changamoto hiyo iwakabili na wamejaribu kuandika barua nyingi kufika kwa mkurugenzi wa Wajiji lakini mpaka sasa changamoto hiyo haijatatuliwa.

“Hatakama barabara hawajatutengenezea basi wajaribu kutuwekea vivuko ili tupite kwa urahisi na pia wasaidie hata watoto wetu watumie kipindi cha Mvua nyingi waweze kwenda shule”,amesema

” kipindi cha Mvua Kuna korongo kubwa lina jaaga Maji lipo block 19 na madhara makubwa yametokea kipindi cha nyuma limesababisha takribani nyumba Nne (4) kubomoka na Watoto pia wanazama kwenye hilo Kongoro”.Amesema Yusufu

Ameongezea kwa kusema kuna eneo ambalo liliathiriwa na Maji Mwaka 2017 watu waliaribikiwa na vitu vyao vya umeme na kusababisha madhara makubwa hata kwa nyumba ambazo ziliwazunguka ziliathiriwa

” 2017 athari hiyo ilitokea na Uongozi ukaambiwana na ulikuja kuangalia athari hiyo hiyo wakasaidia tu kutoa vitu vilivyoathiriwa pamoja na kurekebisha maeneo ya shoti ambayo ilitokea

“Lakini changamoto ile ipo palepale kwasababu walisafisha tu ila kurekebisha hiyo barabara inayokusanya maji na kudababisha korongo kubwa alujafanyiwa kazi mpaka leo”.Amesema Yusufu

Naye Moja kati ya Mwananchi wa Kata hiyo ya Chang’ombe, Zena Bakari ametoa hisia zake kuhusiana na barabara hiyo inawasababishia ukosefu wa usafiri na kutembea umbali mrefu kutafuta usafiri

“Mimi nimfanya biashara na ninatakiwa nidamke asubuhi kwenda kwenye biashara zangu sasa kutokana na hizi barabara zetu yaani hadi bodaboda zinashindwa kuingia huku

” Tunatembea umbali mrefu kutafuta usafiri kwasababu tukisema aje ninapoishi ni mbali na tampa shingapi mpaka ipite hiyo pikipiki? na hili suala sio kwamba Serikali haijui inajua ila wanapotezea tu “.Amesema Bakari

About the author

mzalendoeditor