Featured Kitaifa

TBS KUTUMIA SH.BILIONI 9.9 KUJENGA MAABARA DODOMA NA MWANZA

Written by mzalendoeditor

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS)  Dkt.Athuman Ngenya,akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma  kuhusu  vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS)  Dkt.Athuman Ngenya,akijibu maswali mbalimbali yaliyoulizwa  na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma wakati akitoa taarifa kuhusu  vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23. 

Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,akizungumza wakati wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) likitoa  taarifa kuhusu  vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma.

Mwandishi wa habari kutoka Global TV Mohamed Zengwa,akimuuliza swali  Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS)  Dkt.Athuman Ngenya, (hayupo pichani) wakati akiwasilisha vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma.

Mwandishi wa habari kutoka  Uhuru FM Sakina Abdulmasoud ,akimuuliza swali kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la viwango Tanzania (TBS)  Dkt.Athuman Ngenya, (hayupo pichani) wakati akiwasilisha vipaumbele vya taasisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2022/23 leo Agosti 1,2022 jijini Dodoma.

 

……………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

SHIRIKA  la viwango Tanzania (TBS) limetenga kiasi cha Shilingi billioni 9.9 kwa ajili ya kujenga jengo la maabara katika miji ya kimkakati (Dodoma na Mwanza) ili kusogeza huduma za Shirika karibu kwa wateja na kuongeza ufanisi.

Hayo yamesemwa leo Agosti 1,2022  jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa TBS Dkt.Athuman Ngenya wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu  vipaumbele vya taasisi hiyo amesema lengo la TBS kujenga maabara katika kanda ni kuhakikisha inadhibiti ubora na bidhaa na vibali kupatikana kwa wakati.

Dkt.Ngenya amesema kuwa kwa sasa Maabara ipo Moja tu ya Dar-es-salaam makao mkuu jambo ambalo linasababisha kucheleweshwa kwa huduma.

Dkt.Ngenya amesema kuwa katika kuhakikisha usalama wa vyakula na vipodozi kwa taifa unakuwpo shirika limeona ni vyema kujenga maabara hizo ili kuondasha ile adha iliyopo kwa sasa ya kusafiri kutoka mbali kupeleka bidhaa maabara kuu ya Dar-es-salaam kupima ubora na itasaidia pia kuharakisha maendeleo ya watoa huduma.

“Unakuta mtu anatengeneza mkate wake huko Kagera sasa ili kupitishwa kwa ajili ya kuingizwa sokoni kwa maana ya kuanza kutumika na wananchi ni lazima asafirishe mpaka Dar-es-salaam kwa ajili ya kupimwa ubora sasa embu fikiria kutoka Kagera mpaka Dar-es-salaam hapa katikati inaweza ikatokea chochote ikaoza ama ikapata changamoto sasa unakuwa umepoteza muda”Amesema Dkt.Ngenya

Pia  Shirika limetenga kiasi cha Shilingi billioni 2.7 kwa ajili ya kuimarisha ofisi saba za kanda, mipakani, Bandari ya Mwanza, Tanga, Bagamoyo na Dar es Salaam, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere, Mwanza na Kilimanjaro.

Fedha hizo pia zitatumika kuimarisha ofisi za shirika hilo mipakani ikiwemo Tunduma, Kasumulo, Horohoro, Holili, Tarakea, Namanga, Bandari ya Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwanza, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro,Sirari, Kabanga, Rusumo, Mtukula, Bandari ya bagamoyo, bandari ya Dar es salaam, uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere- Dar, Bandari ya Tanga)

“Pia tutaongeza wafanyakazi na vitendea kazi kwa ajili ya kutoa huduma kwa wakati na kuimarisha zoezi la ukaguzi wa mara kwa mara sokoni ili kupunguza bidhaa hafifu sokoni na hatimaye kuhakikisha wananchi wanapata bidhaa bora na salama” amesema Dkt.Ngenya

Amesema pia shirika hilo limetenga TZS 1.6 Billioni kwa ajili ya kuandaa viwango 630 vya kitaifa katika sekta mbalimbali ili kuwezesha biashara kwa kumpa uhakika mzalishaji wa kupata masoko ya ndani na nje, kumhakikishia mlaji wa mwisho usalama na ubora wa bidhaa atakayotumia ikiwa ni pamoja na kuweka ushindani sawia wa bidhaa katika soko.

Dkt.Ngenya ameongeza kuwa ili kuhakikisha wananchi wanatumia bidhaa zilizo bora na salama Shirika hilo pia limetenga TZS 261 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za usajili wa bidhaa na majengo ya chakula na vipodozi.

 Dkt.Ngenya amebainisha kuwa Shirika hilo pia limetenga TZS 581 Millioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za uthibitishaji wa mifumo ya kiutendaji ambapo kwa sasa TBS imepatiwa ithibati ya kufanya shughuli hiyo na mashirika yanaweza kuthibitishiwa ubora wa mifumo yao ya kiutendaji kupitia hii itasaidia kuhakikisha wananchi wanapokea huduma zilizo bora.

Amesema Katika kufanya shughuli za kuhakiki ubora wa vipimo ili kuhakikisha usahihi wa majibu ya vipimo mbalimbali kutokea maabara, mahospitalini na viwandani na kupelekea watoa huduma au maamuzi kufanya maamuzi sahihi Shirika hilo limetenga TZS 800 Millioni.

Shirika limetenga TZS 1.18 Billioni kwa ajili ya kuimarisha shughuli za ukaguzi wa bidhaa kabla ya kusafirishwa kuja nchini (PVoC) na baada ya kuwasili nchini (Destination Inspection) ili kuhakikisha nchi haiwi jalala la kupokea bidhaa zilizopigwa marufuku au hafifu.

Shirika la viwango Tanznania (TBS) linaendelea na juhudi za kuweka na kutekeleza mikakati mbalimbali ili kuboresha huduma zake kwa lengo la kuwezesha biashara kwa dhumuni la kuinua uchumi wa viwanda kwa kuchagiza uzalishaji wa bidhaa salama na bora hapa nchini kama njia mojawapo ya kuchangia pato la Taifa letu.

Aidha Dkt.Ngenya,amesema kuwa Shirika hilo linaungana na Serikali kuhamasisha Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022.

Kwa upande wake Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari maelezo Gerson Msigwa,amesema kuwa jukumu la serikali  kupitia shirika la viwango Tanzania TBS ni kuhakikisha bidhaa zinazokuja hapa nchini zinakidhivigezo vya kutumika kwa wananchi.

About the author

mzalendoeditor