Featured Michezo

DKT. MSONDE AKEMEA MAMLUKI UMITASHUMTA, UMISETA

Written by mzalendoeditor

Asila Twaha, Tabora

Wasimamizi wa Mashindo ya Kitaifa ya Michezo na Taaluma kwa Shule za Msingi (UMITASHUMTA) na ile ya Sekondari (UMISSETA) wametakiwa kufuata sheria za michezo hiyo kwa kuhakikisha wanaoshiriki ni walengwa pekee.

Michezo hiyo inayotarajia kufanyika Mkoani Tabora, itaanza na michezo ya UMITASHUMTA na kufuatia na UMISETA.

Agizo hilo limetolewa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(Elimu) Dkt. Charles Msonde alipokuwa akizungumza na viongozi wa Baraza la UMITASHUMTA katika Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mkoani Tabora.

Michezo ni somo, hujenga mahusiano mazuri na huibua vipaji kwa watoto hivyo viongozi msije kutia dosari michezo hiyo kwa kutofuata sheria za michezo.

Baadhi ya viongozi kukiuka taratibu za michezo kwa kutafuta washiriki ambao sio wanafunzi na kuwapa nafasi ya kushiriki kwa kutafuta ubingwa usiokua wa kihalali, ninawaelekeza wasimamizi michezo hii ni kwa ajili ya wanafunzi wa shule ya msingi na sekondari.

Dkt. Msonde amewatahadharisha viongozi wa timu za Mikoa kuwa Ofisi ya Rais-TAMISEMI itawachukulia hatua wale watakaobainika kuwatumia wachezaji ambao sio wanafunzi.

” Kama kuna Mkoa umekuja na mamluki muwatoe mapema, kwa tutakao wabaini wameingiza washiriki ambao sio wanafunzi hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao” amesema Dkt. Msonde.

Kwa upande wa Mkurugenzi wa Elimu Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Bw. Ephraim Simbeye amesema washiriki kutoka Mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na wako tayari kwa michezo hiyo.

Timu zote kutoka Tanzania Bara na Zanzibar zimeshafika, nikuhakikishie kuwa tunashirikiana ili kufanikisha michezo hii na kuifanya kuwa na tija kwa shule na kwa wanafunzi.

Naye mshiriki wa michezo hiyo kutoka Mkoa wa Mara, Hurda Marima amesema wapo tayari kushindana na kuhakikisha wanashinda na kuchukua ubingwa sababu wamekuwa wakifanya mazoezi pamoja ya kuwa michezo ni afya lakini wamekuja kushinda sababu hawahofii wapinzani wao.

About the author

mzalendoeditor