Featured Michezo

WAZIRI MCHENGERWA AONGOZA KIKAO CHA UJUMBE WA TANZANIA BIRMINGHAM UINGEREZA

Written by mzalendoeditor

Na John Mapepele
Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe,  Mohammed Mchengerwa  ameongoza
kikao cha maandalizi ya ujumbe wa Tanzania katika kikao cha Mawaziri wa
Michezo wa Jumuiya ya Madola kitakachoanza leo Julai 26 mjini
Birmingham, Uingereza. 
Kikao
hicho ni maandakizi mahususi kabla ya uzinduzi rasmi wa mashindano ya
michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka huu yanayofanyika nchini Uingereza
huku Tanzania ikiwa imeshiriki katika michezo hiyo.
Katika
mashindano hayo kwa mara ya kwanza Serikali imetoa  motisha kubwa kwa
wachezaji watakaofanya vizuri na kurejea na tuzo nchini.
Mhe. Mchengerwa amesema dhamira ya Serikali ni kuhakikisha   michezo inatumika kikakamilifu kuitangaza Tanzania kimataifa.
Aidha,
amesema michezo ni ajira na uchumi mkubwa ambapo amesisitiza wachezaji
wote kuwa wazalendo kujituma kufa na kupona kwa ajili ya taifa la
Tanzania.
Amepongeza
jitihada kubwa zinazofanywa na Serikali chini ya Rais Samia Suluhu
Hassan za kuleta mapinduzi  makubwa kwenye sekta za michezo katika
kipindi kifupi iliyopo madarakani.
Miongoni
mwa motisha hizo amesema  Serikali itatoa kiasi cha  dola  10,000 za
kimarekani kwa mchezaji atakayerejea na medali ya dhahabu, dola 7000 kwa
medali ya Shaba na dola 5000 kwa medali ya fedha.
 Kikao
hicho kimehudhuriwa na Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mhe. Dkt,
Asha-Rose Migiro, Mhe. Mussa Sima ambaye ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu
ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara
ya Michezo Ndugu Saidi Yakubu pamoja na wajumbe kutoka Tanzania.

About the author

mzalendoeditor