Featured Kitaifa

TANZANIA, UFARANSA ZAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akisalimiana na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui wakati wa hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa hotuba yake katika hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akitoa hotuba yake katika hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.

Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui akiwasilisha hotuba yake katika hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 

Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Mizengo Pinda akijadili jambo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk katika hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam 

Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Mizengo Pinda katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk, Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui na Afisa Mtendaji Mkuu NMB Bank, Bibi. Ruth Zaipuna pamoja na maafisa kutoka Ubalozi wa Ufaransa na Wasanii wa muziki wa kizazi kipya

Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk akiteta jambo na Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui wakati wa hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam

…………………………………..

SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Ufaransa zimeahidi kuendeleza ushirikiano katika nyanja za elimu, afya, maji, usafirishaji, kilimo na utalii kwa maslahi mapana ya pande zote mbili.

Ahadi hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mbarouk Nassor Mbarouk aliposhiriki hafla ya kuandimisha Siku ya Taifa ya Ufaransa  iliyofanyika Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Julai 2022.

Balozi Mbarouk alisema Tanzania na Ufaransa zimekuwa na uhusiano mzuri tangu mwaka 1961 na mataifa hayo yamekuwa na ushirikiano katika nyanja za elimu, afya, maji, usafirishaji, mawasiliano, utalii, kilimo, biashara na uwekezaji.

“Ufaransa imekuwa mdau mkubwa katika masuala ya uchumi ambapo kampuni mbalimbali kutoka Ufaransa zimewekeza nchini na zimekuwa zikichangia kutoa ajira kwa watanzania na kuongeza pato la taifa,” alisema Balozi Mbarouk 

Balozi Mbarouk aliongeza kuwa Ufaransa imekuwa mdau mkubwa wa utalii ambapo idadi ya watalii imekuwa ikiongezeka kutoka 25,000 kwa mwaka 2020 hadi 50,000 kwa mwaka 2022.

“Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan imekuwa ikiboresha mazingira ya biashara na uwekezaji ili kuwavutia zaidi wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza  nchini…….pia Serikali inatambua na kuthamini mchango wa wafanyabishara wa Ufaransa katika kukuza sekta uchumi,” alisema Balozi Mbarouk.

Awali Balozi wa Ufaransa nchini, Mhe. Nabil Hajlaoui alisema Ufaransa imefurahishwa na ushirikiano mzuri inaoupata kutoka Serikali ya Tanzania na kuahidi kuwa Ufaransa itaendelea kudumisha uhusiano huo kwa maslahi ya mataifa yote mawili.

Balozi Hajlaoui aliongeza kuwa Ufaransa itaendelea kushirikiana na Tanzania kuunga mkono juhudi mbalimbali za kukuza maendeleo ya kijamii, kisiasa na kiuchumi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania.

“Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Ufaransa kwa muda mrefu nawaahidi hapa kuwa uhusiano huu tutaendelea kuudumisha na kuulinda wakati wote,” alisema Balozi Hajlaoui

Balozi Hajlaoui aliongeza kuwa Ufaransa inaridhishwa na jitihada za Tanzania katika kuhakikisha usawa wa kijinsia katika jamii, uhuru wa demokrasia, kulinda amani na usalama ndani na kwenye kanda.

About the author

mzalendoeditor