Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akifurahia jambo kutoka kwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndugu Godwin Mkanwa (kulia) mara baada ya kumaliza hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (Bara) Ndugu Christina Mndeme akiteta jambo na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akisalimiana na Kamisaa wa Sensa ya Watu na Makazi, Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akihutubia wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Viongozi wa matawi na mashina waliochaguliwa 2022 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Jakaya Kikwete Convention.
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiongozana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dodoma Ndugu Godwin Mkanwa, Naibu Katibu Mkuu CCM (Bara) Ndugu Christina Mndeme wakikagua mradi wa vyumba 172 vya maduka vya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Dodoma .
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Daniel Chongolo akiweka jiwe la msingi ufunguzi wa mradi wa ujenzi wa vyumba 172 vya maduka katika viwanja vya Barafu Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Picha na Adam H. Mzee/ CCM Makao Makuu)
……………………………………..
Na Eva Godwin-DODOMA
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),Daniel Chongolo ametoa wito kwa ngazi zote za Watendaji kuanzia Tawi,kata, Wilaya na Mikoa yote nchini kuwekeza nguvu kwenye uwekezaji na utendaji wa uchumi wa chama hicho.
Ameyasema hayo Julai 13,2022 katika Kongamano la Mafunzo ya Uongozi na uwajibikaji katika mada za Itikadi,Elimu ya Sensa na makazi,Tehama na Usajili wa Wanachama pamoja na Masuala ya Ulinzi na Usalama kwa Viongozi wa Chama kuanzia ngazi za Mashina Jijini Dodoma.
Amesema uboreshwaji wa uchumi kwenye chama itasaidia mambo yote kuwa rahisi na wataepuka kukimbiana katika vikao vya kujenga masuala yote ya msingi.
” Ni lazima kwanza tuboresha uchumi ili mambo yatunyookee, tukiboresha uchumi wa chama chetu mambo yetu yote yatakuwa rahisi na tutaacha kukimbiana kwenye masuala ya Msingi”,amesema
“Na hivi karibuni tutakusanya mikoa ambayo imelala lala tunawachukua waje kujifunza waone Mikoa mingine inavyofanya vizuri Mkoa wa Dodoma ni moja kati ya Mikoa inayofanya vizuri katika suala la Uchumi”.Amesema Chongolo
Aidha amesisitiza kwa Wagombea kuepuka suala zima la rushwa katika kipindi hichi cha uchaguzi ikiwi ni kiapo cha Mwanachama ambapo ni ahadi katika chama.
“Tunaposoma ahadi ya Mwananchama kila Mmoja aliapa kuwa rushwa ni adui wa haki na pale mlikuwa mkimaanisha kuwa rushwa ni jambo lisilokubalika,kila Mmoja atumie yale mema yake ambayo anaona ataweza kujinadi “,smesema
“Tufanye Kampeni kwa kutumia nguvu zetu bila kutengenezeana uongo na uzushi pamoja na kutengenezeana ajali tusipende kuwekeana chuki sisi kwa sisi”.Amesema Chongolo
Hata hivyo Chongolo ameagiza vikao vitakavyo jadili majina ya wahusika katika ngazi usika kutoona aibu kuchukua hatua kwa watu watakao kiuka maagizo halali yaliyowekwa na Chama.
“Hatuwezi kuwa chama ambacho tunatoa maelekezo kwaajili ya kutoa fursa kwa Watu wote kuwa sawa kwenye kugombania kinyang’anyiro cha kugombea nafasi mbali mbali na baadhi ya wachache kuona wao wanapembe ndefu kuliko Mmiliki wa pembe usika”,amesema
“Chama ndicho chenye dhamana na nafasi, Mtu ukiona unataka dhamana hiyo usipo fuata maagizo na maelekezo yetu utakuwa hututakii jambo zuri na utakuwa unatulazimisha kuchukua hatua na hatutosita kuchukua kwasababu utakuwa ameyataka mwenyewe”.Amesema Chongolo