Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFANYA UTEUZI TENA

Written by mzalendoeditor

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amemteua Dkt. Kedmon Elisha Mapana kuwa Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

Dkt. Mapana anachukua nafasi ya Bw. Godfrey Lebejo Mngereza ambaye amefariki dunia. 

Kabla ya uteuzi huo Dkt. Mapana alikuwa Mhadhiri Mkuu, Idara ya Sanaa Bunifu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Uteuzi huu unaanza mara moja.

About the author

mzalendoeditor