Mwenyekiti wa mkutano wanayasansi, ambaye pia Mtaalamu wa Utafiti wa Ikolojia ya Panya kutoka Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Panya cha chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Rhodes Makundi akiongea na waandishi wa habari mkoani Arusha.
Wanasayansi walizofanya utafiti uliosaidia kuondoa matatizo ya Panya kwa binadamu wakiwa wameshika tuzo katika kati akiwa ni Profesa Rhodes Makundi.
………………………………………………………………
NA NAMNYAK KIVUYO,ARUSHA
Wanasayansi kutoka nchi 50 Duniani wameadhimia kuweka umuhimu katika utafiti wa Panya kwenye magonjwa yanayoambukizwa kutoka kwao ikiwemo ugonjwa wa Tauni na Leptospirosis kutokana na magonjwa hayo kujitokeza katika mada 16 walizozijadili katika mkutano wa saba wa kimataifawa wa bayolojia ya panya na udhibiti wa Panya Duniani uliofanyika kwa siku siku nne mkoani Arusha
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Mwenyekiti wa mkutano huo, ambaye ni Mtaalamu wa Utafiti wa Ikolojia ya Panya kutoka Kituo cha Umahiri cha Utafiti wa Panya cha chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Prof. Rhodes Makundi alisema kuwa magonjwa hayo yamekuwa maarufu zaidi na yanatakiwa kufanyiwa utafiti wa kutosha.
Profesa Makundi alieleza kuwa pia Panya wameanza kuwa muhimu kwenye maeneo mengi Duniani kutegemeana na vitu ambayo binadamu wanavifanya ambapo wamekubaliana kufanya utafiti zaidi kuhusu mahusiano ya Panya na viumbe vingine vinavyokaa kwenye mazingira yake.
“Kingine ni namna ya kuwadhibiti Panya kwakuwa inaelekea wanadhidi kuwa muhimu katika magonjwa na kilimo kwahiyo lazima tuendelee kufanya utafiti wa ndani zaidi kwani tumegundua kuwa utafiti ambao umejitokeza sasa hivi ni utafiti wa kuzuia Panya kuzaana na katika Afrika, Tanzania ndio inayoongozwa kwenye utafiti huo,” Alisema Profesa Makundi.
Alifafanua kuwa eneo lingine waliloona ni muhimu ni matumizi ya Panya kwa faida ya binadamu ambayo hiyo inalenga utafiti wanaofanya Sokoine unaohusu kutumia Panya katika kutambua mabomu na Magonjwa kama kifua kikuu ambapo pia Kuna utafiti unaoendelea.
“Tunaweza kusaidia binadamu kwa mfano kigundua wenye kifua kikuu lakini pia maeneo yenye mabomu kama maeneo yaliyopata shida ya vita miaka iliyopita,” alisema.
Aliendelea kusema kuwa pia jopo la Wanasayansi hao limetambua mchango wa baadhi ya maprofesa kwa kazi nzuri waliyoifanya kusaidia binadamu kuondoa matatizo ya Panya ambapo wamepewa tuzo mmoja wapo akiwa ni yeye Profesa Rhodes Makundi kwa kufanya kazi kwa takriban miaka 40 pamoja na wengine wawili ambao wamefanya kazi kwa takriban miaka 30 ambapo mkutano huo umehudhiriwa na watu zaidi ya 100 huku zaidi ya 80 wakishiriki kwa njia ya mtandao.