Featured Kitaifa

DC LONGIDO AISHUKURU SHIRIKA LA AL ATA’A CHARITABLE FOUNDATION KWA KUTOA MATIBABU YA MACHO WILAYANI HUMO.

Written by mzalendoeditor

Aliyekaa ni mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu akifanyiwa vipimo vya macho, kulia kwake ni Mkurugenzi mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation Ahmed Elhamrawy na kushoto ni Nicolaus Kiwia Mteknolojia mkuu wa macho kutoka hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha maunt Meru akimfanyia vipimo.

 Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu akiongea katika zoezi la utoaji wa matibabu ya macho katika kituo Cha afya cha wilaya hiyo kwa udhamini wa shirika la Al Ata’a Cheritable Foundation.

 Mkurugenzi mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation Ahmed Elhamrawy akimkabidhi mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu miwani mara baada ya kufanyiwa vipimo na kugundulika kuwa na tatizo.

 Mkurugenzi mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation akiongea na wananchi katika zoezi la utoaji wa huduma ya macho iliyotolelewa na shirika hilo kwa wananchi wa wilaya ya Longido.

Mteknolojia mkuu wa macho kutoka hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Maunt Meru Nicolaus Kiwia akimfanyia mmoja wa wananchi vipimo vya macho.

picha ya pamoja ya viongozi wa wilaya ya Longido, Al Ata’a Cheritable Foundation na baadhi ya wataalamu kutoka hosipitali ya Maunt Meru.

Mratibu wa macho mkoa wa Arusha Lawrence Mremi akiongea katika zoezi Hilo la utoaji wa huduma za matibabu za macho.

Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za matibabu ya macho katika kituo Cha afya cha Longido.

……………………………………..
NA NAMNYAK KIVUYO, ARUSHA
Mkuu wa wilaya ya Longido Nurdin Babu ameishukuru shirika la Al Ata’a Charitable foundation linalofadhiliwa na Qatar Charity ya nchini Qatar kwa kutoa huduma ya macho kwa wananchi kutoka kata mbalimbali za wilaya hiyo huku akisisitiza kuwa jicho lina umuhimu zaidi katika mwili wa binadamu.
Akiongea katika zoezi la upimaji na utoaji wa matibabu ya macho yaliyodumu kwa zaidi ya siku tatu katika kituo cha afya Longido, Babu alisema kuwa shirika hilo limehangaika kutafuta fedha kwaajili ya kuwasaidia wahitaji wasio na uwezo wa kumudu gharama za matibabu na kwa kuwatibia binadamu Mungu anawafungulia mambo mengi zaidi.
“Tunawashukuru sana kwa jambo hili kubwa ambalo mmeamua kutufanyia na niwaambie ndugu zangu nafasi hizi haziji mara kwa mara bali zinakuja kwa bahati, wananchi tunatakiwa tujitoe kwani kwa mazoea watu wengi hatuna utaratibu wa kwenda hosipitali kwaajili ya kucheki afya ya micho ila mpaka mtu apate madhara makubwa kama vile kutoona ndio aende hosipitali,” Alisema Babu.
Alifafanua kuwa wananchi wanatakiwa wakacheki mara kwa mara kwani katika mwili kila kiungo kina umuhimu wake lakini jicho lina umuhimu zaidi hivyo wananchi waendelee kujitokeza kwa wingi lakini pia amewaomba wafadhili hao jambo hilo lisiwe la mwisho bali wawakumbuke na  wakati mwingine.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa Al Ata’a Cheritable Foundation Ahmed Elhamrawy alisema kuwa huduma wanayoitoa kwa jamii mbalimbali ni endelevu ambapo wana programu ambazo wanampango wa kufanya katika sekta ya afya katika magonjwa ya kisukari, moyo na magonjwa ya njia ya upumumuaji ambapo kwa upande wa macho wanakuwa na kambi kwaajili ya macho tuu ambapo wanawaona watu 1000 na kuwafanyia upasuaji watu 200 wa mtoto wa jicho.
Alifafanua kuwa wanawafikia watu kulingana na utaratibu wanaopewa na wizara ya Afya juu ya tatizo husika kwani tatizo la macho ni tatizo kubwa na hasa linahitaji mtu apate matibabu katika hatua za mwanzoni na mtu akichelewa tatizo linazidi kuwa kubwa  lakini katika maeneo mengine watu wanashindwa kwenda hosipitali kutokana na ukosefu wa huduma hiyo ndio maana kama tasisi wameenda na vifaa kwaajili ya kupima na kuwatibu ikiwemo kufanya upasuaji ili kuweza kupambana na changamoto zilizopo.
“Mpaka sasa tumeshafanya hizi kambi za macho  mara nne katika mikoa mbalimbali hapa Tanzania, ikiwemo mikoa ya Kigoma, Pwani, Dodoma na Sasa tupo Arusha katika eneo hili la Longido na tunampango wa kwenda Monduli na tumeshafanya operesheni na chekap  kama 800 na matibabu haya tunatoa bure ambapo katika hosipitali za serikali mtu akiumwa anaweza kupata matibabu kwa laki moja na nusu hadi mbili  na huku hosipitali binafsi ikiweza kuwa hata zaidi ya milioni moja,”Alisema Ahmed.
Kwa upande wake Mratibu wa macho mkoa wa Arusha Lawrence Mremi alisema kuwa mpaka Sasa wameweza kufikia watu 600 katika wilaya hiyo na zoezi bado linaendelea ambapo Wilaya hiyo Ina shida ya wagonjwa wengi wa macho kutokana na eneo lenye kuwa kame na upungufu wa maji  pamoja na kuwa na uhaba wa wataalamu wa macho ambapo wilaya nzima ina wataalamu wawili tuu.
Alisema kuwa kwa kuzingatia ukubwa wa tatizo la macho kwa watu hao ambapo kuna wenye Trakoma, kuna wanaohitaji matibabu ya macho, wanaohitaji miwani na upasuaji wa mtoto wa jicho ambapo yote hayo kwa uthamini wa Al Ata’a Cheritable Foundation watapata matibabu ambapo visababishi vya magonjwa ya macho ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi juu ya utunzaji wa macho kwa kujikinga na mambo mbalimbali yanayoweza kudhuru jicho.
Nao baadhi ya wananchi walionufaika na huduma hiyo, Naparakwo Laizer alisema kuwa jicho lake lilikuwa likiwasha na baadae  kuwa analifikicha mara kwa mara ndipo  ulifika wakati jicho hilo likawa halioni tena lakini amefika katika kituo hicho cha afya na kukuta huduma hiyo ambapo amepata vipimo na baada ya vipimo iligundulika anahitajika kufanyiwa upasuaji wa jicho hilo na kufanyiwa jana, na leo amerudi kuendelea na matibabu na anaona vizuri sasa huku akiendelea kutumia dawa.
Naye mwananchi kutoka kata ya  Kimokowa  Saruni Ole Kuku alisema kuwa amekuja na mke wake kupata huduma ya macho ambapo mke wake baada ya vipimo amepewa dawa ambayo baada ya kumaliza kuitumia atatakiwa kwenda katika hosipitali ya rufaa ya mkoa wa Arusha Mount Meru kwaajili ya matibabu zaidi lakini pia yeye baada ya vipimo amepewa miwani, aidha  ameishukuru kwa kuletewa huduma hiyo ambayo imewasaidia kwani wametibiwa na kupata ushauri utakasaidia kuendelea kutunza macho yao.

About the author

mzalendoeditor