Featured Kitaifa

WAZIRI MASAUNI ATETA NA WAJUMBE WA BODI YA SHIRIKA LA UZALISHAJI MALI LA JESHI LA POLISI, JIJINI DAR ES SALAAM

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Prof. Suffian Bukurura (kushoto), wakati alipokuwa anawasili kuzungumza na Wajumbe wa Bodi hiyo, Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na Wajumbe wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, katika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Suffian Bukurura, na wapili kulia ni Katibu wa Bodi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Massawe.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Prof. Suffian Bukurura, wakati alipokuwa akizungumza katika kikao cha Waziri huyo na Wajumbe wa Bodi, kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto meza kuu ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Christopher Kadio, alipokuwa akizungumza katika Kikao cha Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Suffian Bukurura

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati), akimsikiliza Katibu wa Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP), John Massawe alipokuwa akizungumza katika Kikao cha Bodi hiyo, kilichofanyika Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Prof. Suffian Bukurura

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio, akisalimiana na Mkurugenzi wa Kitengo cha Huduma za Sheria wa Wizara hiyo, Marlin Komba (kulia), wakati alipokuwa anawasili katika Kikao cha Bodi ya Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Polisi, kilichofanyika katika ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay Jijini Dar es Salaam, leo. Kushoto ni Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Lucas Mkondya, na wapili kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ACP Jumanne Muliro. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

About the author

mzalendoeditor