Featured • Kitaifa

LUSWETULA KUONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA KUJADILI CHANGAMOTO ZA MAENDELEO AFRIKA

Written by Alex Sonna

Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akiongoza kikao cha maandalizi ya Tanzania kushiriki katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jesca Mboho, akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Mkurugenzi wa Ubunifu, Utafiti na Maendeleo, Tume ya Taifa ya Mipango, Dkt. Evodius Kanyamyoga, akifafanua jambo ajenda zinazotarajiwa kujadiliwa katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Mwambata Siasa, Ubalozi wa Tanzania, Nigeria, Bw. Allen Kuzilwa akizungumza katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akimsikiliaza Mchumi kutoka Wizara ya Fedha, Bi. Jesca Mboho, aliyekuwa akitoa taarifa kuhusu ushiriki wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Naibu Waziri wa Fedha, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akiagana na Ujumbe wa Tanzania baada ya kikao cha maandalizi ya Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Cotonou, Benin)

Na Farida Ramadhani, WF, Cotonou, Benin

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar, ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 35 wa Bodi ya Magavana wa Taasisi ya Kujenga Uwezo Afrika (The African Capacity Building Foundation – ACBF) na Mkutano wa Afrika wa Taasisi za Tafiti na Majadiliano ya Sera (Africa Think Tank Summit – ATTS), utakaofanyika jijini Cotonou, Jamhuri ya Benin tarehe 28 hadi 30 Oktoba 2026.

Mkutano huo utakao wakutanisha viongozi wa Serikali, watunga sera, watafiti, wataalamu, sekta binafsi na washirika wa maendeleo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika, unalenga kujadili nafasi ya tafiti, uimarishaji wa uwezo wa taasisi na mageuzi ya sera katika kukabiliana na changamoto za maendeleo barani Afrika, hususan katika sekta ya nishati, uwekezaji, ukuaji wa uchumi na uboreshaji wa huduma kwa wananchi.

Tanzania inatarajiwa kujumuika na wadau wengine kujadili upatikanaji na ugharamiaji wa nishati ya umeme kwa kuangalia namna sekta ya nishati inavyoweza kutumika kama kichocheo cha kuongeza uzalishaji, ushindani na ukuaji wa uchumi jumuishi.

Kupitia majadiliano yatakayofanyika, Tanzania inatarajiwa kupata fursa ya kubadilishana uzoefu na wadau mbalimbali kuhusu namna ya kuvutia uwekezaji katika miundombinu ya nishati, kuboresha mifumo ya usimamizi wa sekta ya umeme na kutumia teknolojia zinazoweza kuongeza ufanisi wa uzalishaji na usambazaji wa nishati ili kujenga sekta ya umeme iliyo imara na inayoweza kuchangia kikamilifu katika mageuzi ya kiuchumi barani Afrika.

Sambamba na masuala ya nishati, mikutano hiyo inalenga kuimarisha nafasi ya tafiti na ushahidi wa kitaalamu katika uandaaji na utekelezaji wa sera za maendeleo ambapo Tanzania inatarajia kupata maarifa mapya, kuboresha upangaji wa mipango na kuimarisha uwezo wa taasisi katika kutekeleza vipaumbele vya Taifa vilivyoanishwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa 2050 (Dira 2050).

About the author

Alex Sonna