Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete awasili Jijini Tanga kwa ziara ya kikazi ya siku moja ambapo katika ziara hiyo amefungua Kikao Kazi cha Maafisa Sheria na Maafisa Rasilimaliwatu, kuzungumza na Watumishi wa Umma wa mkoa huo pamoja na kukagua utekelezaji wa maendeleo ya ujenzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Kampasi ya Tanga.
Mhe. Waziri Kikwete amepokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian.
