Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akizungumza na wajumbe kutoka Tanzania watakaoshiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika Sekta ya Afya, alipowasili jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akisikiliza maelezo kutoka kwa ujumbe wa Marekani ulioongozwa na Mratibu Msaidizi wa Masuala ya Fedha wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Omar Kebbeh, alipowasili jijini Nairobi kushiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika Sekta ya Afya.

Mratibu Msaidizi wa Masuala ya Fedha wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Omar Kebbeh, akieleza mikakati mbalimbali ya ufadhili wa miradi alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), baada ya kuwasili jijini Nairobi, Kenya.

Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), akipitia agenda za Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika Sekta ya Afya alipowasili jijini Nairobi, Kenya. Kulia ni Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabiri Seleman.

Wajumbe kutoka Tanzania wakifuatilia maelezo wakati wa mkutano kati ya Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), na ujumbe wa Marekani ulioongozwa na Mratibu Msaidizi wa Masuala ya Fedha wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Omar Kebbeh.

Ujumbe kutoka Marekani ukiongozwa na Mratibu Msaidizi wa Masuala ya Fedha wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Omar Kebbeh (kulia), ukiwa katika mazungumzo na Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), alipowasili jijini Nairobi, Kenya, kushiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika Sekta ya Afya.
(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Fedha, Nairobi, Kenya)
Na. Peter Haule, WF, Nairobi, Kenya
Naibu Waziri wa Fedha, Mhe. Laurent Luswetula (Mb), amewasili jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kushiriki Jukwaa la Mazungumzo ya Ngazi za Juu la Mawaziri wa Fedha kuhusu kuimarisha uwekezaji wa pamoja katika Sekta ya Afya, akimwakilisha Waziri wa Fedha, Mhe. Balozi Khamis Mussa Omar (Mb).
Mkutano huo unaofanyika katika Hoteli ya JW Marriott, Nairobi, unawakutanisha Mawaziri wa Fedha kutoka nchi mbalimbali za Afrika zilizoingia Hati za Makubaliano (MoU) na Serikali ya Marekani kuhusu ufadhili wa masuala ya afya.
Jukwaa hilo linatoa fursa kwa Mawaziri hao kubadilishana uzoefu na kujadili mbinu bora za kuongeza uwekezaji katika Sekta ya Afya, kuimarisha ushirikiano wa kimataifa, pamoja na kuoanisha Sera za Fedha na Afya katika nchi za Afrika zilizoingia makubaliano hayo na Serikali ya Marekani.
Baada ya kuwasili Nairobi, Mhe. Luswetula alikutana na ujumbe kutoka Marekani ulioongozwa na Mratibu Msaidizi wa Masuala ya Fedha wa Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Bw. Omar Kebbeh.
Katika mazungumzo yao, ujumbe huo ulimpa maelezo ya awali kuhusu ufadhili katika sekta za maendeleo, pia alipitishwa katika agenda za mkutano huo na kupata taarifa muhimu kuhusu ushiriki wake katika mkutano kutoka kwa Afisa Usimamizi wa Fedha Mwandamizi wa Idara ya Fedha za Nje, Wizara ya Fedha, Bw. Jabiri Seleman.
Mkutano huo unatarajiwa kuwa sehemu muhimu ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za Afrika na Serikali ya Marekani katika kuongeza uwekezaji na upatikanaji wa rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya Sekta ya Afya.