DODOMA
BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limempitisha Mheshimiwa Deogratius John Ndejembi kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupata kura zote 324 zilizopigwa, sawa na asilimia 100.
Uamuzi huo umefanyika baada ya jina la Ndejembi kuwasilishwa Bungeni kwa ajili ya kupata ridhaa ya Wabunge, ambapo kura hizo zimeonyesha kuungwa mkono kwa pamoja kwa uteuzi wake kushika nafasi hiyo ya juu ya uongozi wa Taifa.