Featured Kitaifa

RAIS SAMIA AFUNGUA MSIKITI WA JAMI’UL ISTIQAMA BUKOBA

Written by mzalendoeditor
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili katika Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera kwa ajili ya kufungua rasmi Msikiti huo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikata utepe kuzindua rasmi Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiondoa kitambaa kuashiria kuzindua rasmi Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Istiqama mara baada ya kufungua  rasmi Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Viongozi wa Dini pamoja na Wananchi kwenye Hafla ya ufunguzi wa Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Tuzo Mwakilishi wa Balozi wa Oman Nchini kwa Niaba ya Balozi kwa kutambua Jitihada zake katika Nyanja mbalimbali za Maendeleo hapa nchini, wakati wa Hafla ya ufunguzi wa Msikiti wa JAMI`UL  ISTIQAMA Bukoba mjini  Mkoani  Kagera
……………………………………………….
Na Silvia Mchuruza.Bukoba,Kagera.

Ni katika ziara ya siku tatu mkoani kagera rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania mh.Samia Suluhu Hassan amefanya   ufunguzi rasmi wa msikiti wa jami’ul istiqaama Bukoba  mkoani kagera.

Akizungumza katika uzinduzi huo ulifanyika katika msikiti wa istikama uliopa mkabara na stendi kuu ya mabasi mjini Bukoba  mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania amewataka viongozi wa jumuiya ya istiqaama kutumia Kodi za freemu za biasha katika msikiti huo wa istiqaama kukarabatiwa na hata kutumia fedha hizo kukarabatiwa pia mabomba pale yanapo haribika.
Pia amezisisitiza Jumuiya za kimaendeleo kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Kila jumiya, asasi zote za kidi kuleta maendeleo ya  pamoja hapa nchini na kuwataka watu kuendelea kujiandaa zaidi katika ujio wa zoezi la sensa nchi lengo likiwa Ni kutambuana na kujuana nchi inao watu wangapi au wananchi wangapi.
Aidha nae Shekhe Abubakar Zuber Ally shekhe mkuu wa Tanzania amesema jumuhiya ya istiqaam imekuwepo toka enzi za wajerumani lakini jumuiya ambayo imeishi vizuri na wananchi na kutoa huduma ya kijamii katika mkoa wa kagaera.
Pia ameongeza kwa kusema kuwa wale watu wanaodhani kuwa sensa aipokwenye dini watakuwa  wanapotosha watu kwani sensa ipo katika vitabu vyote vya dini na kuwataka mashekhe wowote nchini  wahahakikishe wawanazungumzia suala la sensa na kulieleza vizuri.
Shekhe Zuberi amewaonya watu wanaofanya mauajo hovyo hapa nchini kuacha tabia hizo walejee kwenye dini kwani wanailetea jamii matatizo na huzuni jambo ambalo alikubaliki kwa serikali na  kwa viongozi wa dini.
” Tuache kufanya mauaji ya ovyo kwani Ni dhambi kujiua au kuua mtu yeyeyote tuludi kwenye dini tujue kuwa mungu yupo kwani kufanya mauaji ya Aina yoyote Ni dhambi na tukumbuke nchi yetu Ni ya amani na utulivu Sasa tusiuvunje utulivu wetu”
 Kaimu Barozi wa serikali ya omani Dr.Salimu binsaif Al harbi amesema Jumuiya ya  istiqaam imejipanga kushirikiana na serikali ya Tanzania kuchimba visima vya maji katika shule mbalimbali hapa nchi pia ameongeza kuwa Jumuiya ya istiqaam imepokea maombi ya ujenzi wa msikiti mkubwa mwingine hapa Tanzania katika jiji la dodoma.
Pia ameshukuru kwa uongozi wa Jumuiya ya istiqaam Tanzania kwa usimamizi Bora na mzuri kwa kusimamia ujenzi wa msikiti  huo.
Mwakilishi wa istiqaama shekhe seif bin seif 
Kutoka Tanzania ameshukuru serikali ya omani kwa kuwawezesha fedha za kumaliza ujenzi wa msikiti huo uliopo mjini Bukoba mkoani kagera.
Amesema Ujenzi wa msikiti huo ulianza mwaka  2019 na msikiti ambao  ulikuwa  wa zamani uliojengwa mwaka 1956 ulikuwa mdogo lakini msikiti wa sasa una jumla ya vyumba vya madrasa 6 vya madrasa hii Ni kwa ajili ya kuwafanya vijana wa kislamu kujifunza zaidi kuhusu mafundisho ya  dini ya kislamu na Sasa msikiti huu umetimiza miaka 166.
Pia amesema Jumuiya hiyo Inamiliki shule 14 za chekechea , msingi , na sekondari vituo viwili vya afya  hapa nchini na lengo la Jumuiya kwa Sasa Ni kujenga shule kubwa ya secondary katika jiji la dar es salaam kwani ndi po wana jumuiya wengi wa istiqaama walipo.
 Amemuomba mh.rais kuipati jumuhiya ya istiqaama eneo kubwa katika jiji la dodoma kwa ajili ya kujenga kituo Cha Islamic senta jijini dodoma kitakacho wasaidia zaidi pia wanna dodoma.

About the author

mzalendoeditor